Habari Mseto

Deacons yatimua wafanyakazi 93 kubana matumizi

January 23rd, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Deacons East Africa imewafuta kazi wafanyikazi 93 kwa lengo la kudhibiti gharama.

Kampuni hiyo pia inalenga kuwaachilia wakurugenzi wake kwa lengo la kuimarisha uaminifu katika hatua ya kuifufua.

Wasimamizi wa kampuni hiyo, Peter Kahi na Atul Shah wakati wa mkutano na wanahabari walisema kundi ndogo litaisaidia kuimarika.

Hii ni kuambatana na changamoto za kibiashara zinazoendelea kushuhudiwa nchini, walisema wasimamizi hao.

“Nyakati zimebadilika na kumekuwa na hali ya kutokuwa na uhakila, hilo sio suala la kutilia shaka,” alisema Bw Shah kutoka PKF Consulting.

Kwa sasa, kampuni hiyo ina wafanyikazi 60 katika matawi yake yote ikilinganishwa na 153 awali.

Kampuni hiyo itawaajiri wakurugenzi wapya pamoja na mkurugenzi mkuu, nafasi inayoshikiliwa na Wahome Muchiri.

Pia, Deacons inalenga kuhamisha afisi kuu kutoka Norfolk Towers kwa lengo la kudhibiti zaidi gharama.

Matawi yamesalia nane kutoka 12 huku wasimamizi hao wakipendekeza kuuzwa kwa matawi ya Uganda na Rwanda kwa lengo la kudhibiti deni.