Dondoo

Demu aachia mume watoto na kurudia ex aliyeomoka ghafla

June 13th, 2024 1 min read

SHANZU, MOMBASA

Na JANET KAVUNGA

MWANADADA aliyekuwa akiishi hapa na mumewe aliwaacha watoto wake na kurudi kwa mumewe wa zamani akisema alikosea kumuacha kwa sababu ya umasikini.

Mwandada aliolewa na mumewe wa sasa miaka kumi iliyopita na wakajaliwa watoto wawili walio na umri wa zaidi ya miaka mitano.

Majuzi, alikutana na mumewe wa zamani akiendesha gari la kifahari na baada ya kufanya uchunguzi akabaini jamaa aliomoka na hakuoa tena.

Hapo ndipo aliamua kumrudia na jamaa alipokubali, akaamua kuacha watoto na baba yao huku mashogake wakimlaumu kwa kuwa kujawa na tamaa ya mali.

“Unatumia wanaume vibaya kiasi cha kuacha watoto wako kwa sababu mumeo wa zamani amepata pesa ilhali ulimuacha kwa sababu ya umasikini, utajuta,” mama mmoja alimwambia.