Dondoo

Demu achemkia baba kwa kumkopesha mumewe wa zamani hela


KIPUSA wa hapa alimchemkia babake kwa kumsaidia mumewe licha ya wawili hao kutengana kwenye ndoa yao.

Kulingana na duru, mrembo na mumewe walikosana kuhusiana na tofauti za ndoa na kipusa akarudi kwa wazazi wake.

Juzi, kipusa huyo alipata habari kamili kuwa babake alimkopesha mumewe hela chungu nzima aimarishe biashara yake changa.

“Mbona unampa pesa huyo mtu ilhali tumeachana na yeye kabisa? Koma kutupa pesa zako kwa mtu asiyeaminika,” kidosho akawaka kwa hamaki.

“Mumeo ni kijana ninayemheshimu kwani ni mwanabiashara hodari sana. Amekuwa rafiki yangu hata kabla muoane,” buda akamjibu bintiye na kumwarifu kuwa anawaombea moto wa mapenzi kati yao uwake tena.