Dondoo

Demu adai mume amempuuza chumbani, eti kazi ni kusomasoma vitabu tu!

June 5th, 2024 1 min read

Na JANET KAVUNGA

MWANADADA wa hapa amelalamika kuwa mumewe anapenda kusoma sana wakiwa chumbani badala ya kumshughulikia.

“Ninashindwa chumba cha kulala ni cha kazi gani kwa mtu na mkewe kwa kuwa mume wangu anapenda kuzama katika vitabu au laptop yake kusoma nikimhitaji anipashe joto,” demu aliambia wenzake wakiwa saluni.

“Nimeshindwa na tabia yake ambayo inanikosesha raha. Ni kama jamaa haelewi maana ya kuwa na mke,” alieleza.

Kulingana na mwanadada, sio eti jamaa anasomea mtihani bali huwa anachangamkia vitabu vya hadithi.

“Nimemwambia asipobadili tabia nitatafuta mtu wa kujaza nafasi anayoacha katika maisha yangu ya mahaba. Nahitaji kupapaswa sio kupuuzwa,” alisema.