Dondoo

Demu ajiondoa kwa chamaa cha vidosho wanyemeleaji wa mabwana

January 5th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

MTWAPA, KILIFI

DEMU wa hapa alijiondoa kutoka kikundi cha vipusa wenzake, mmoja wao alipomuonjesha asali mpenzi wake.

Demu aliwatumia wenzake ujumbe wa kujiondoa kama mwanachama wa kikundi akiwalaumu baadhi ya wanachama kwa kunyemelea wapenzi wa wengine.

“Siwezi kuwa katika kundi moja na mtu aliyemnyemelea mpenzi wangu na kumgawia tunda. Nina ushahidi wa kutosha kwamba alimrushia mpenzi wangu chambo, akamnunulia pombe akalewa na akakodisha chumba wakalala wakirushana roho. Kuanzia sasa, nimejiondoa katika kikundi chenu na msipochunga atapita na wapenzi na waume zenu,” demu alilalama.

Wenzake waliahidi kufanya uchunguzi wao huru na kuapa kumchukulia hatua mhusika wakithibitisha madai yake.