Michezo

Demu amlilia Mbappe ampachike mimba

May 20th, 2019 1 min read

NA MASHIRIKA

KICHUNA Alicia Aylies amemtaka mshambuliaji nyota wa PSG, Kylian Mbappe kumfunga bao haraka upesi wakati wanapoendelea na mipango ya kurasimisha uhusiano wao kupitia harusi ya kukata na shoka baadaye mwaka huu.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, Mbappe ambaye anahemewa pakubwa na Real Madrid, alikiri kwamba kinachotawala zaidi mawazo yake kwa sasa ni maandalizi ya sherehe za harusi zitakazomshuhudia hatimaye akifunga pingu za maisha na Alicia, mrembo aliyetawazwa mshindi wa Miss France mnamo 2017.

Ingawa Mbappe alitaka maandalizi ya hafla hiyo yasalie kuwa siri kubwa, Alicia aliudokezea ulimwengu wa udaku kuhusu mpango wao kwa kurushia mitandaoni picha alizopigwa kwa pamoja na mwanasoka huyu ambaye ushawishi wake unazidi kuhisika sana uwanjani Parc des Princes.

Kwenye picha hiyo, Alicia alipania kuonyesha zaidi kidole chake kilichovishwa pete ya thamani kubwa japo hakuweka bayana iwapo ni pete ya uchumba kutoka kwa Mbappe.

Hata hivyo, aliandika, “Nipo tayari kukupokeza rasmi funguo za mzinga wangu na kinachosalia tu ni sisi kuweka sawa mipango ya ndoa ambayo sina shaka itafana sana. Fanya hima nikuzalie dume na jike.” Kwa upande wake, Mbappe alisema kwa sasa kinachomuumiza kichwa ni kuteua msimamizi wa ndoa yao.