Dondoo

Demu awaka kupata picha za mume akila bata na manyanga katika ufuo

April 23rd, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

BAMBURI, MOMBASA

JAMAA mmoja wa hapa alikuwa na wakati mgumu baada ya mkewe kupata picha alizopigwa majuzi akijivinjari na mpango wa kando ufuoni.

Jamaa huyo ni bingwa wa michepuko licha ya kuwa na mke mrembo ambaye amekuwa akipuuza mistari ya wanaume wengi mafisi wanaomnyemelea.

Juzi, mwanadada alikuwa akidurusu mtandao wa Facebook alipoona picha za mumewe akijivinjari na demu mwingine ufuoni kusini mwa pwani.

“Alipopata picha hizo zilizochapishwa na kipusa asiyemjua, alimkabili mumewe. Kumbe una mpenzi wa kando! Kuanzia leo nataka uamue kitu kimoja, unipe talaka ulete huyo mpenzi wako. Hata mimi naweza kupata dume la kula raha nalo,” demu alimkaripia mumewe.

Jamaa aliingiwa na baridi akaomba msamaha japo alisisitiza demu huyo hakuwa mpenzi wake bali rafiki wa kawaida tu.