Depay na Coutinho wabeba Barcelona dhidi ya Villarreal ligini

Depay na Coutinho wabeba Barcelona dhidi ya Villarreal ligini

Na MASHIRIKA

BARCELONA walifunga mabao mawili katika dakika za mwisho na kucharaza Villarreal 3-1 katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Frenkie De Jong alifungulia Barcelona ukurasa wa magoli katika dakika ya 48 kabla ya Samuel Chukwueze kusawazishia Villarreal katika dakika ya 76. Hata hivyo, Memphis Depay aliwarejesha Barcelona uongozini katika dakika ya 88 kabla ya Philippe Coutinho kuzamisha chombo cha wenyeji wao sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa.

Licha ya kusajili ushindi wao wa kwanza ugenini muhula huu, Barcelona wangali katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa jedwali la La Liga kwa alama 23, sita nyuma ya Real Sociedad. Ushindi wa Barcelona uliendeleza rekodi ya kutopigwa kwa kikosi hicho chini ya kocha mpya Xavi Hernandez ugani Camp Nou tangu aaminiwe fursa ya kuwa mrithi wa mkufunzi Ronald Koeman.

You can share this post!

Palmeiras wazamisha Flamengo na kutwaa taji la tatu la Copa...

Atalanta yapiga Juventus nyumbani kwa mara ya kwanza tangu...

T L