Habari Mseto

Dhamana ya Sh100,000 kwa kuoa msichana wa miaka 16

June 18th, 2020 1 min read

ALEX NJERU

Mwanamme wa miaka 20 katika eneobunge la Tharaka, Kaunti ya Tharaka Nithi ameshtakiwa katika korti ya Marimanti kwa kosa la kumuoa msichana mwenye miaka 16 wa Darasa la Nane.

Mshtakiwa huyo Peter Murithi alikiri kosa hilo mbele ya hakimu mkuu Peter Maina.

Korti iliamuru kwamba mshukiwa huyo aendelee kuzuiliwa mpaka Jumapili wiki ijayo wakati hukumu litakapotolewa. Alipewa fursa ya kulipa dhamana ya Sh100,000.

Baba wa Murithi, Samuel Gichungu Makembona mama wa Msichana huyo pia walishtakiwa kwa kuruhusu ndoa hiyo.

Wawili hao pia watazuiliwa rumande hadi Jumatatu wakingoja hukumu ama walipe dhamana ya Sh 100,000 pia.

Kesi za ndoa za mapema, mimba za mapema na dhuluma zingine dhidi ya wasichana zimetokea wakati huu wa janga la corona ambapo huku shule zikiwa zimefungwa watoto wengi wanarandaranda vijijini.