Dhana ya Utamaushi inavyokuzwa katika ‘Chozi la Heri’

Dhana ya Utamaushi inavyokuzwa katika ‘Chozi la Heri’

JUMA hili tutashughulikia namna wahusika mbalimbali katika riwaya ya ‘Chozi la Heri’ walivyotamauka.

Ridhaa anatamauka kufuatia mauko ya mkewe Terry, Wanawe Tilla na Mukeli, Lily mkaza mwanawe na mjukuu wake Becky.

Aidha, anatamauka nyumba zake zinapobomolewa na nyingine kuchomeka.

Pete anatamauka maishani baada ya kupata watoto watatu akiwa mchang. Anaazimia kujitia kitanzi ili aepuke majukumu yake.

Kijana aliyevalia shati lililoandikwa Hitman ametamauka kwani elimu yake haijamsaidia.

Aidha, hata baada ya viongozi kuwaahidi kazi, baada ya uchaguzi, wanawaambaa wananchi waliowapigania hata kupata vyeo.

Hazina ya vijana kukosa kupatikana na hata mashamba kunyakuliwa na mabwenyenye. Analipua gari na kulichoma kwa kutamauka.

Selume anatamauka kwa kutuhumiwa kumuunga mkono mpinzani mkuu wa mumewe, analazimika kutengana na mumewe na hata kumuacha mtoto wake. Anatamauka kwa kushindwa kumtunza mwanawe Sara.

Kipanga anatamauka kwa kutengwa na babake wa kambo. Jambo hili linamfanya kujiingiza katika ulevi na hata kulazwa katika hospitali ya Mwanzo Mpya.

Vijana katika chuo kikuu wanatamauka kutokana na gharama ya maisha na kujiingiza katika ulevi unaosababisha mauko ya wengine.

Sauna anapobakwa na babake wa kambo, Bwana Maya,kuavishwa mimba na mamake, anatamauka na kuwa na hali ya kutaka kulipiza kisasi kwa ulimwengu na baadaye kuhusika katika ulanguzi wa watoto.

Baada ya kifo cha Lily na Becky, Mwangeka anatamauka kiasi cha kukosa kuoa tena kwa miaka mitatu.

Kwa mujibu wa Tila, wahafidhina wametamauka kiasi cha kukataa uongozi wa kawaida. Wanampigia kura Mwekevu kwani uongozi uliokuwepo umekuwa wa watu wanaojitakia makuu.

Mamake Sauna ametamauka kiasi cha kuona kuwa hawezi kumchukulia hatua Maya kwa kitendo cha uhayawani alichomtendea Sauna.

Zohali anakata tamaa baada ya kupachikwa ujauzito, aendapo nyumbani kwao, anatwikwa ujakazi jambo ambalo linamfanya kutoroka kwao na hata kusema kuwa wazazi wake wameaga dunia.

Lunga Kiriri-Kang’ata anapohamishwa na kuelekezwa mlima wa Simba,anatamauka anapoachwa na mkewe na kusababisha kuaga dunia kutokana na ukiwa aliokuwa nao.

Naomi, mkewe Lunga Kiriri-Kang’ata, anapoamia Mlima wa Simba, anatamauka na kuamua kumwacha mumewe pamoja na watoto wake.

Neema anapompoteza mtoto wake, anatamauka kwa kuwa hangekuwa na uwezo wa kumpata mtoto mwingine.Anaposimangwa, anazidisha kukata tamaa, hadi anapompanga Mwaliko.

Shamsi naye anatamauka baada ya kufutwa kazi, licha ya kuwa msomi, hakushughulika kutafuta kazi nyingine,ila alijiingiza katika ulevi na utegemezi.

Subira anatamauka baada ya kupitia mateso mengi kutoka kwa mama mkwe wake. Anaamua kuiacha familia yake na kujifilia mjini baada ya kunywa kinywaji kikali.

Joyce Nekesa

Kapsabet Boys High School

  • Tags

You can share this post!

‘Wiki ya Lugha za Kiafrika’ ni mwamko mpya kuhusu...

Aliyekuwa mpuliza kipenga wa EPL, Mark Clattenburg,...

T L