Habari Mseto

Diamond kukamatwa akiandaa shoo Kenya

December 20th, 2018 1 min read

NA MWANDISHI WETU

MSANII maarufu kutoka Tanzania Diamond Platnumz huenda akashtakiwa kwa jinai na serikali ya nchi hiyo endapo ataandaa shoo ya muziki wake nchini siku ya kuvuka mwaka katika hafla ya Wasafi Festival Jijini Nairobi.

Bodi ya kusimamia muziki Tanzania (Basata) ilitangaza hayo, baada ya kuwapiga marufuku Diamond pamoja na msanii Rayvanny kutotumbuiza kwa nyimbo zao ndani na nje ya Tanzania, baada yao kukashifu marufuku ya wimbo wao wa ‘Mwanza.’

Msanii huyo anatarajiwa kuandaa shoo 3 usiku wa kuvuka mwaka Embu, Mombasa na Nairobi.