Bambika

Diamond Platnumz aelekea ‘Zenji’ kumuomba Zuchu msamaha

February 24th, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

MWANAMUZIKI mmiliki wa lebo ya WCB Wasafi Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz, yuko njiani kuelekea visiwani Zanzibar, nyumbani kwa kina Zuchu kumuomba msamaha warudiane.

Zuchu ni binti ya malkia wa Taarab, Khadija Kopa.

Katika taarifa yake kwenye mtandao mmojawapo wa kijamii, mwanamuziki huyo ametangaza yuko njiani kuelekea nyumbani kwa kina Zuchu visiwani Zanzibar–Zenji–kuomba radhi baada ya kushauriwa kuchukua hatua hiyo muhimu.

“Kaka yangu Haji Manara jana alinishauri niache kiburi niende Zanzibar nikaombe msamaha pengine nitaweza (ku)rudiwa… (Baada ya kutafakari) kwa muda mrefu nikagundua yuko sahihi,” akasema Diamond.

“Nami niko njiani kuelekea Zanzibar kulitekeleza hili. Nahitaji sana mawazo yenu kuhusu ubunifu wa kuomba msamaha, lakini pia uwepo wenu kwenye Full Moon Party Kendwa Rocks Zanzibar leo ili kunisaidia kulikamisha hili,” akaongeza.

Hatua hii ya msani huyo mkubwa wa Bongo ilijiri saa chache tu baada ya Zuchu kutangaza kukatika kwa uhusiano wao wa kimapenzi uliodumu kwa takriban miaka miwili.

Manara ni rafiki wa karibu wa Diamond.

Mapema mwaka huu 2024, Manara alimwalika mwanamuziki huyo kuwa mgeni wa heshima wakati alimposa mpenziwe.

“Naomba huyu awe wa mwisho sasa,” alishauri Diamond katika sherehe hiyo.

Pia, Diamond alichukua fursa hiyo kumtetea Manara baada ya kuondolewa kwenye usimamizi wa soka nchini Tanzania.

Bosi huyo wa WCB alisema kuwa kuondelwa kwa Manara hakukuwa na msingi wowote kwa sababu “Manara alikuwa akifanya kazi nzuri.”