Didmus Barasa asema anayefaa kukamatwa ni Raila

Didmus Barasa asema anayefaa kukamatwa ni Raila

NA WANGU KANURI

MBUNGE wa Kimilili Didmus Barasa amewanyooshea kidole wanasiasa wanaoshawishi polisi kumkamata baada ya kubandika posta za kampeni kwenye gari la serikali.

Akizungumza kwenye mkutano wa kisiasa, Barasa alisema, “Wale watu ambao wanasema nimefanya makosa kwa kutumia gari la CDF. Mimi ni mbunge ambaye yupo kwenye kiti. Raila hajachagulia, alijiapisha peke yake, yeye ni mhalifu na anatumia magari 22 ya serikali.”

Akiongeza kuwa atakubali kukamatwa pindi tu Raila ajaposhikwa, Bw Barasa alisema, “Kabla hamjakuja kumkamata huyu kijana ya mjane, kamata Raila Amolo Odinga kwanza yeye afungwe kwanza ndio mje mnikamate mimi.”

Barasa alijikuta lawamani baada ya kubandika posta ya kampeni iliyoonyesha picha yake na mgombea rais kwa chama cha UDA, William Ruto kwenye gari la hazina ya maendeleo ya eneobunge (CDF).

Mbunge huyo pia alitoa nambari ya usajili ya gari hilo ambayo ni GK948J na kusajili gari lilo hilo nambari KBS 709D.

Hata hivyo, mkuu wa polisi katika eneobunge la Kimilili Mwita Maroa alisema kuwa gari hilo lilipatikana nyumbani kwa mbunge Barasa Jumanne asubuhi katika kijiji cha Nasianda lakini wafanyikazi wakawakataza maafisa hao kufika pale.

Bw Maroa vile vile alisema kuwa ni kinyume na sheria kwa mtu kutumia magari ya serikali kwa manufaa yake mwenyewe au kwa kampeni.

  • Tags

You can share this post!

LISHE: Chagua chakula chenye manufaa kwa mtoto

KAULI YA MATUNDURA: Kiswahili ni ufunguo wa milango ya...

T L