DIMBA: Harusi tunayo! Ya Trapp na Izabel

DIMBA: Harusi tunayo! Ya Trapp na Izabel

IMEKUSANYWA NA CHRIS ADUNGO

MWANAMITINDO Izabel Goulart amesema maandalizi ya ndoa kati yake na kipa matata wa Ujerumani, Kevin Trapp, yaelekea kukamilika.

“Mambo ni shwari na mpango kwa sasa ni kutafuta wapambe wa harusi itakayofanyika mwezi huu,” akaandika Izabel kwenye mtandao wake wa kijamii.

Izabel, ambaye ni raia wa Brazil, alianza kumfungulia Trapp, 31, buyu lake la asali mnamo 2018.

Demu huyo mwenye umri wa miaka 37 aliwahi pia kunogesha kipindi cha fasheni cha Victoria Secret mnamo 2017.

Katika mahojiano awali na gazeti la The Sun, Izabel alikiri kwamba kinachomdumisha sana kwa Trapp ni nguvu nyingi za ujana za kipa huyo, ambaye hushiriki naye miereka ya siri chumbani angalau mara tano kila wiki.

Trapp kwa sasa anadakia kikosi cha Eintracht Frankfurt katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

Aliwahi kunyanyua mataji mawili ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) akivalia jezi za Paris Saint-Germain (PSG) kati ya 2015 na 2018.

Mbali na kuwaniwa na vikosi vya Ligi Kuu Uingereza (EPL), Trapp anahusishwa pia na uwezekano mkubwa wa kujiunga na Real Betis ya Uhispania au Hertha Berlin ya Ujerumani mnamo Januari 2022.

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Kylian Mbappe

UDA yaondoa mamlakani maafisa walioteuliwa majuzi

T L