DIMBA: Kiganjo Kings wanatambua bidii ya mchwa itawajenga

DIMBA: Kiganjo Kings wanatambua bidii ya mchwa itawajenga

Na JOHN KIMWERE

CHANGAMOTO zimekuwa chungu nzima, lakini hazijazuia wachezaji wa Kiganjo Kings kutia bidii, kwani lengo lao ni kutua Ligi Kuu (KPL) katika miaka minne ijayo.

Kiganjo Kings ni miongoni mwa timu 12 zinazoshiriki mechi za Kundi B kuwania taji la Central Regional League (CRB) muhula huu.

“Tunazidi kukabili wapinzani wetu kwenye mechi za mkumbo wa pili ambapo tunaamini kuwa tutapata matunda mema na kupiga hatua kwenye msimamo wa kipute hicho,” meneja wa kikosi hicho, Samuel Kiarie alisema na kuongeza kuwa wanafahamu hakuna shughuli rahisi.

Meneja huyo anashikilia kuwa ndio mwanzo wanashiriki mechi za kinyang’anyiro hicho lakini wanaamini kwamba wachezaji wao wanayo nafasi kupaisha mchezo wao na kutinga miongoni mwa nafasi bora katika jedwali.

“Ndio mwanzo tunashiriki michuano yenye ushindani mkubwa ambapo tunaendelea kujifunza mengi dhidi ya wapinzani wetu,” kocha wa kikosi hicho, Joseph Kiaritha alisema.

Aliongeza kuwa timu za maeneo hayo zinamilikiwa na kampuni tofauti hali inayoziweka vizuri kuzima juhudi za wenzao eneo hilo.

Anatoa wito kwa wachezaji wake kabla wajitahidi kukabili wenzao wala wasikubali kulaza damu kiulani.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Stephen Marubu anatoa wito kwa wahisani popote walipo wajitokeze kuzipiga jeki timu zinazokuja ili kuendeleza mtindo wa kukuza wachezaji chipukizi.

You can share this post!

MBWEMBWE: Kigogo Chiellini ana noti za kukausha bahari nzima

DIMBA: Mwatate All Stars FC yapania kushinda taji