Divock Origi abanduka Liverpool na kuingia katika sajili rasmi ya AC Milan

Divock Origi abanduka Liverpool na kuingia katika sajili rasmi ya AC Milan

Na MASHIRIKA

ALIYEKUWA fowadi wa Liverpool, Divock Origi, ameingia rasmi katika sajili rasmi ya AC Milan ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) bila ada yoyote.

Nyota huyo raia wa Ubelgiji aliye na usuli nchini Kenya, alibanduka ugani Anfield mwishoni mwa msimu wa 2021-22 baada ya kuchezea Liverpool mechi 175 na kufungia miamba hao mabao 41 tangu ajiunge nao mnamo 2014.

Origi, 27, anakumbukwa kwa kufungia Liverpool mabao muhimu katika mechi za haiba kubwa, ikiwemo ile iliyowavunia ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2019.

AC Milan wanonolewa na kocha Stefano Pioli walitawazwa wafalme wa Serie A mnamo 2021-22 baada ya kusubiri taji hilo kwa zaidi ya miaka 10. Waliwapiku Inter Milan waliokuwa mabingwa watetezi kwa pointi mbili pekee kileleni mwa jedwali.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

Serikali ya Tanzania yakemea ulanguzi wa watoto walemavu

Beth Mugo apinga uamuzi wa IEBC kutumia KIEMs pekee...

T L