Habari Mseto

Diwani afariki baada ya kuugua kwa muda mfupi

November 10th, 2020 1 min read

RUTH MBULA NA FAUSTINE NGILA

Diwani wa Kiamokama Kennedy Michira Mainya amefariki, amethibisha kiongozi wa wengi bungeni la  Kisii Timothy Ogugu Ijumaa. Alifariki  baada ya kuugua kwa kuda mfupi na kulazwa hospitalini Alhamisi.

Bw Ogugu alisema kwamba Bw  Mainya alifariki Jaumapili Narok  alipokuwa akikibizwa hospitalini Nairobi kwa kutumia Abulensi,alichokuwa akiugua akikutajwa.

“Mainya  alikuwa mwenye afya hadi Alhamisi alipolazwa hospitali ya Oasis Kisii”,alikuwa anaogezwa pumzi lakini hali yake ikaadhofika kalazimika kuhamishwa hospitali nyingine.

Mkurugenzi wa maswala ya afya Kisii Daktari Richard Onkware alisema kwamba Diwani huyo alikuwa amepimwa virusi vya corona lakini matokeo hayakuwwa yametoka bado.

Ujumbe kutoka kwa  bunge hilo ulisema kwamba Bw Mainya alifariki baada ya kugonjeka kwa muda mfupi kwamba kaunti hiyo ilikuwa imepoteza kiogozi wa kiukweli.

“Alikuwa kwa ambelensi akipelekwa Nairobi kufuatia matatizo ya kupumua .Alikuwa amelazwa hospitali ya Oasis kwa muda wa chini ya wiki moja.

Spika wa Bunge hilo David Kombo alimtaja kiogozi huyo kuwa kiogozi aliyekuwa mtulivu na aliyekuwa anajua kazi yake”.