Habari Mseto

Diwani motoni kuhusu kifo cha mkewe

June 8th, 2020 1 min read

NICHOLAS KOMU

Diwani mmoja katika Kaunti ya Nyeri alijipata mashakani huku akilazimika kujibu kuhusu kifo cha mkewe. Mwili wa mkewe diwani wa wadi ya Konyu Erick Mwangi Wamumbi ulipatikna ndani ya bwawa Jumatatu asubuhi.

Mwili wa Catherine Nyambura ulionekana na mkazi akielekea kazini.

Kisa hicho kwanza kilikuwa kimeripotiwa kama kujitoa uhai lakini baada ya kufuatiliwa ikangunduliwa kwamba mwathiriwa hakua na majeraha yeyote, polisi walisema.

“Wito ulitoka kwa umma kwambalkuna mwili wa mwanamke ulioonekana katika bwawa la Hanwe.

“Tuliutoa mwili huo na tukaupeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Karatina,” mkuu wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Mathira James Barsa alisema.

Mwili huo ulitambuliwa na diwani aliyeambia wenzake kwamba mke wake alikuwa amejitoa uhai..

Jumanne, maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya upelelezi [DCI] walienda kwenye bwawa hilo kufanya uchunguzi zaidi.

Bw Barasa alisema kwamba hakukuwa na ripoti ya kupotea kwa mtu yeyote kinyume na maelezo ya diwani huyo.

“Baada ya upasuaji wa mwili tutajua kilichopelekea kifo cha Nyambura,” afisa wa polisi alisema.

Wapelelei walielezea Taifa Leo kwamba kulikuwa na barakoa mbili zilizokuwa zimetupwa karibu na bwawa hilo na zitatumika katika uchunguzi.

Mashaidi walisema kwamba walisikia mabishano kati ya mwanamke na mtu asiyejulikana karibu na bwawa hilo.

Diwani huyo kufikia sasa hajatoa taarifa yeyote kuhusiana na kisa hicho isipokuwa taarifa ya rambirambi aliyotoa kwenye mtandao wa kijamii.