Habari Mseto

Diwani Peter Chomba afariki

October 10th, 2020 1 min read

NA DENNIS LUBANGA

Kaunti ya Uasin Gishu inaomboleza kifo cha diwani wa wadi ya Huruma Peter Chomba. Mbunge wa Kapseret  Oscar Sudi alithibitisha kifo hicho akisema kwamba Chomba alifariki kwenye hospitali ya Eldoret alipokuwa akikitibwa Jumamosi baada ya kupata matatizo ya kupumua.

Mbunge huyo Sudi alisema kwamba diwani huyo alianguka bafuni wiki iliyopita na kwamba alikuwa anaenda hospitali kutibiwa.

Bw Chomba alizungumza na wezake wakiwemo kiogozi wa wengi wa kaunti hiyo ya Uasin Gishu Josphat Lowoi na diwani wa Langas Francis Muya na kuwaeleza kuhusiana na hali yake ya kiafya alisema Bw Sudi.

Diwani huyo alikibizwa hospitali na mkewe Jumamosi asubuhi na kufariki alipofikishwa hospitalini.

Spika wa kaunti hiyo ya Uasin Gishu David Kiplagat alitaja kifo hicho kuwa cha kutisha.

“Huku tukiendele kutoa risala za rambirambi kwa familia ya tutaotao taarifa kuhusiana na hili baadaye Jumamosi,”alisema Spika.

Mbunge wa zamani wa Turbo Elisha Buseenei alimwomboleza Bw Chomba akisema alikuwa kiongozi mpenda amani.

Naibu Gavana wa kaunti hiyo ya Uasin Gishu Daniel Chemno alisema kwamba kaunti hiyo itampa diwani huyo mazishi ya heshima.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA