DKT FLO: Chunusi sehemu ya siri ni tatizo la kiafya?

DKT FLO: Chunusi sehemu ya siri ni tatizo la kiafya?

Mpendwa Daktari Flo,

Nilikumbwa na chunusi moja lenye maumivu makali eneo linalozingira sehemu yangu ya siri. Bada ya siku chache, lilitoweka. Je, hii yaweza kuwa onyo la tatizo la kiafya? Christine, Nairobi

Mpendwa Christine,

Sababu kuu ya chunusi zenye maumivu katika sehemu za siri ni vinyweleo vya nywele za sehemu hii (mahali ambapo nywele huchomoka kwenye ngozi) vinapozibwa na bakteria au vitu vingine.

Kuna baadhi ya watu watu ambao huathirika pakubwa hili linapotokea, kutokana na wepesi wa kingamwili, au kwa sababu ya mabadiliko ya kihomoni.

Ni tatizo ambalo hukumba watu wanene zaidi kwa wingi na kamwe halitokani na uchafu. Wakati mwingine uvimbe huu hauishi, lakini kuna nyakati ambapo hutokomea na kuacha makovu.

Kichocheo kingine pia chaweza kuwa kunyoa. Baada ya kunyoa, nywele huanza kuota na kupenyeza tena kwenye vinyweleo. Ncha kali za nywele hudunga vinyweleo kabla ya kuonekana nje ya ngozi.

Hii yaweza sababisha sehemu iliyoathirika kuvimba, kuasha na kubadilisha rangi na kuwa nyekundu. Hali hii inafahamika kama pseudo-folliculitis.Wakati mwingine sehemu hii yaweza pata maambukizi.

Hii yaweza tokea mahali popote ambapo nywele zimenyolewa au kung’olewa, ikiwa ni pamoja na uso, makwapa, kinena na miguuni.Tiba sahili ni kuacha nywele ziendelee kuota au kuzichenga tu badala ya kuzinyoa kabisa.

Unaweza tumia krimu ya kunyoa au kutumia utaratibu wa kudumu wa kuondoa nywele wa laser au electrolysis. Nywele zilizoota ndani ya uvimbe zaweza tolewa kwa utaratibu kwa kutumia kikoleo.

Kuna baadhi ya krimu ambazo zaweza saidia kupunguza uvimbe kama vile steroid cream, dawa za kukabiliana na chunusi, krimu za viua vijasumu ikiwa kuna maambukizi, au tembe za viua vijasumu, ikihitajika.

Unapoendelea kupokea matibabu, waweza pimwa kubaini ikiwa una maambukizi mengine.Mpendwa Daktari,Inawazekana kuanza kushuhudia ishara za ujauzito wiki moja tu baada ya utungaji mimba kutokea?

Jane, MombasaMpendwa Jane,Naam inawezekana kuanza kuonyesha ishara za ujauzito baada tu ya wiki moja, japo sio jambo la kawaida.

Pindi baada ya utungaji mimba, yai lililorutubishwa husafiri kutoka mirija ya fallopian tubes hadi kwenye uterasi, na kujitungisha ukutani, siku ya sita au ya saba baadaye.

Hili linapofanyika, huenda ukashuhudia damu kidogo kuvuja au kuumwa na tumbo. Huenda baadhi ya watu wakashuhudia uchovu na maumivu kwenye matiti wiki moja baada ya utungaji mimba, na dalili zingine kama vile kichefuchefu na kutapika, maumivu ya kichwa, na tumbo kuvimba siku au wiki chache baadaye.

You can share this post!

Chanjo ya corona ilivyo changamoto kwa wazee

Wataalamu wanaonya dhidi ya kutumia tembe za P2 kiholela