DKT FLO: Mbinu asili za kuzuia kisukari ni salama?

DKT FLO: Mbinu asili za kuzuia kisukari ni salama?

Na DKT FLO

Mpendwa Daktari,Jamaa yangu mmoja anaugua kisukari na amechoka kutumia dawa za kisasa.

Hivi majuzi alifichua kwamba amekuwa akitumia mchanganyiko wa juisi ya mboga na mdalasini. Kinachoshangaza ni kwamba anasema amekuwa akipata nafuu. Mbinu hizi za kiasili ni salama?Fanuel, Nairobi

Mpendwa Fanuel,Kisukari huanza mfumo unaokabiliana na sukari mwilini unapokumbwa na hitilafu. Ni hali ambayo huendelea muda unavyozidi kusonga, na pindi mfumo huu unapofeli kabisa, hali ya kawaida haiwezi rejeshwa.

Dawa husaidia mwili kukabiliana na sukari na iwapo matumizi yatasitishwa au pasipo kuzingatia maelekezo ya daktari, kiwango cha sukari katika damu kitaongezeka na kusababisha matatizo mengine kama vile figo kushindwa kufanya kazi, hali ambayo yaweza sababisha upofu.

Kuna matibabu mengine mbadala ambayo yamethibitishwa kupitia utafiti na uchunguzi thabiti. Kwa upande mwingine, mengine hayahimiliwi kisayansi, kumaanisha hakuna utaratibu hususan wa kuyatumia. Kwa ufupi, sio jambo la busara kutumia mbinu ambazo hazijathibitishwa kisayansi.

Mpendwa Daktari,Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa na jipu katika sehemu inayozingira uke wangu hasa ninapokaribia hedhi. Nini chasababisha tatizo hili?Neema, Mombasa

Mpendwa Neema,Uvimbe unaojitokeza kila mara kwenye sehemu ya siri waweza kuwa wasababishwa na maambukizi kwenye vinyweleo.Kuna baadhi ya watu wanaokumbwa na shida hii pengine kutokana na kingamwili dhaifu au kwa sababu ya mabadiliko ya kihomoni wakati wa hedhi.

Tatizo hili pia huwakumba watu wenye uzani mzito.Kumbuka kwamba hali hii haiwezi kuambukizwa na haisababishwi na uchafu. Wakati mwingine uvimbe huu hukoma bila tiba yoyote na kuacha kovu.

Kwa upande wako ambapo uvimbe huu umekuwa kwa wiki kadhaa sasa, unahitaji kumuona daktari au mtaalamu wa ngozi ili upewe viua vijasumu na dawa za maumivu. Mtaalamu huyu atakuelekeza iwapo unahitaji matibabu zaidi.

  • Tags

You can share this post!

City Stars, Homeboys na Bandari zawika ligi ikianza kushika...

Dawa mpya yathibitishwa kuwa na uwezo wa kupunguza makali...

F M