DKT FLO: Nitaongezaje unene kifuani na makalio?

DKT FLO: Nitaongezaje unene kifuani na makalio?

Mpendwa Daktari,

MIMI ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30. Nahisi kwamba mimi ni mwembamba sana. Mbinu zipi salama za kuongeza unene hasa katika sehemu ya makalio na kifua?

Aminata, Mombasa

Mpendwa Aminata,

Wembamba unamaanisha kwamba kimo chako kikilinganishwa na uzani wako (BMI) kiko chini.

Huenda hii ikasababishwa na jeni, au kwa sababu mwili wako unatumia nguvu nyingi kufanya kazi za kila siku.

Aidha hali hii yaweza tokana na sababu kwamba hauli chakula cha kutosha, au endapo unajihusisha na shughuli nyingi.

Pia yaweza kutokana na maradhi fulani au unakumbwa na tatizo la kiakili.

Huku baadhi ya watu wakiongeza au kupunguza uzani kuambatana na lishe au masuala mengine wanayokumbana nayo, uzani wa wengine haubadiliki kwa urahisi.

Hii mara nyingi ni kutokana na jeni, hali ambayo kwa bahati mbaya haiwezi badilishwa. Ni vyema kuwa na uzani usioongezeka au kupungua kila mara. Dhana kwamba unene ni ishara ya afya njema ni potovu. Ikiwa uzani wako ni thabiti hasa katika kiwango kizuri kiafya, basi haupaswi kuingiwa na wasiwasi.

Dumisha lishe bora, kula viwango vidogo vya vyakula kila mara, fanya mazoezi na jiepushe na tabia zisizoambatana na afya njema kama vile kuvuta sigara au kulewa kupindukia.

Unaweza tafuta ushauri kutoka kwa mtaalamu wa lishe kuhusu vyakula vya kula na kwa viwango vipi. Hakuna jinsi ya kupima kwamba uzani unaoongeza utaelekea kwa kifua na makalio. Umbo la mwili kwa upande mwingine hutegemea na jeni.

You can share this post!

BENSON MATHEKA: Hatua zichukuliwe upesi kukabili matatizo...

DKT FLO: Uvimbe pajani, tiba ipi?

T L