DKT FLO: Uvimbe pajani, tiba ipi?

DKT FLO: Uvimbe pajani, tiba ipi?

Mpendwa Daktari,

NILIKUWA na uvimbe kwenye paja ambapo ulianza kujitokeza mapema mwaka jana. Miezi michache iliyopita nilifanyiwa upasuaji kuundoa na kurejea hali ya kawaida. Shida ni kwamba wiki kadhaa zilizopita ulianza kuchipuka tena. Tiba ni ipi?

Arthur, Mombasa

Mpendwa Arthur,

Uvimbe huu waweza kuwa uotaji usio wa kawaida wa baadhi ya seli na tishu au kutokana na mkusanyiko wa uowevu. Huenda uvimbe huo ukasababisha kansa. Njia ya kipekee ya kujua nini kinachosababisha uvimbe huu ni kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. Utaratibu huu ungefanywa baada ya uvimbe wa kwanza kuondolewa. Ikiwa utaratibu huu ulifanywa, basi sampuli ingechukuliwa kutoka kwa uvimbe huu.Pindi aina ya uvimbe huu ikitambulika, basi daktari atakuambia ikiwa waweza tibiwa au ikiwa kuna njia ya kuizuia kuchipuka tena.

  • Tags

You can share this post!

DKT FLO: Nitaongezaje unene kifuani na makalio?

CHARLES WASONGA: Serikali iweke mikakati ya kuzuia mlipuko...

T L