DNA yaonyesha mjukuu wa Moi ndiye baba ya watoto anaopinga kuwalea

DNA yaonyesha mjukuu wa Moi ndiye baba ya watoto anaopinga kuwalea

Na JOSEPH OPENDA

UCHUNGUZI wa chembechembe za damu (DNA) umedhihirisha kuwa mjukuu wa hayati Daniel Moi, ndiye baba mzazi wa watoto wawili anaolaumiwa kwa kukataa kuwatunza.

Matokeo hayo yaliyowasilishwa katika korti moja ya Nakuru yalionyesha kuwa Bw Collins Kibet Moi ndiye baba mzazi wa wototo hao wawili.

Bw Kibet alishtakiwa na mkewe wa zamani, Gladys Jeruto Tagi mnamo Aprili 2021 kwa kutowajibikia watoto wao.

Hata hivyo, Bw Kibet alikanusha madai hayo na kutaka uchunguzi wa DNA ufanywe ili kuthibitisha ikiwa hao ni watoto wake kweli kabla awashughulikie.

Katika kesi hiyo, Bi Jeruto alimtaka Bw Kibet kumlipa Sh1 milioni kila mwezi kama pesa za kuwalipia watoto karo na kuwakimu.

Ripoti ya uchunguzi wa DNA uliofanywa katika maabara ya Lancet Kenya, Nakuru, ilithibitisha kuwa Bw Kibet alikuwa baba mzazi wa watoto hao wawili kwa asilimia 99.

“Bw Collins Kibet Moi ni baba mzazi wa watoto hao wawili,” ikasoma ripoti.

You can share this post!

FAO yajikakamua kuchangisha fedha kuokoa kaunti 23...

TAHARIRI: Serikali ikabili baa la njaa mapema