DOMO: Bibiye atapatapa kujipandisha dau!

DOMO: Bibiye atapatapa kujipandisha dau!

NA MWANAMIPASHO

SIJUI kama umegundua, Huddah Monroe Njoroge kaanza mitikasi ya kurudi kwenye anga za kuzungumziwa.

Shangazi ameshagundua kuwa taarifa zake siku hizi ndio hatuna kabisa. Zile enzi za kumsema magazetini na sijui kwenye blogu ndio zimepotea. Kelele zake anazipayukia Insta kwa mamiloni ya mashabiki wake akitegemea zitafika mbali lakini zinaishia pale.

Kwa binadamu wa hulka kama yake, wanapenda kuzungumziwa sana. Ndio maana namshukuru sana yule dume aliyempanda mbegu Vera Sidika. Siku hizi Insta ina amani kidogo.

Sio kila siku tunaamka kukutana na makalio ya Vera kama ilivyokuwa utaratibu kabla ya ujio wa mtoto. Leo hii yupo bize kunyonyesha, makalio atatuanikia saa ngapi?

Ila huyu Huddah ndio kawashinda madume kumsemeka mhogo wa kumzalisha. Bibiye anaogopa soko linadidimia. Hazungumziwi kama zamani.

Kaichukua kazi hiyo soshiolaiti Amber Ray ambaye haogopi kuuza kwa mwenye dau kubwa mnadani. Tena anakiri hilo kwa sauti kubwa.

Hajali kwamba ana mtoto wa kiume anayetosha kumgeuza nyanya kama akipenda.

Corazon Kwamboka naye mnamwona, alishazunguka sana na wazungu, akitubabaisha na kizungu chake, mwisho wa siku alikutana na mwalimu wa P.E aliyemsemeka wana wawili.

Siku hizi katulia analea akijitahidi kuwa kielelezo bora kwa wanawe. Wote hawa walianza hizi mitikasi na Huddah ila wao wameshakubali muda wao sokoni ndio kama vile unaelekea kikomo. Wameanza kujipanga kwa maisha mengine.

Sasa kabaki Huddah ambaye anajitahidi kubakisha udamshi damshi wake. Ameshazunguka sana. Ameshajaribu kuanzisha ‘Fans Only’ ila kama vile biashara hiyo ilifeli baada ya kukosa kuwaonyesha mashabiki waliolipa, walichotaka kuona. Huyo sasa bibiye anatapatapa kujipandisha dau.

Lala salama

Juzi alidai anamtamani Ferdinard Omanyala na haiwezi kuwa kesi kumpa mechi kama akitaka. Unaweza kuona ni kwa nini anammezea mate. Mwanzo ni jinsi mjomba alivyopiga gym na kuunyoosha mwili wake. Pili ni mkwanja.

Siku zote Omanyala amekuwepo, imekuwaje leo ndio kagundua kuwa jamaa ana mvuto?

Lakini Omanyala kamjibu kwa kusema, hamtaki. Alikwenda hatua na kusema urembo wa Huddah haufikii wa mkewe. Sina uhakika wa hilo, ila wajua tena urembo upo kwa mwenye macho.

Nataka kuamini Huddah aliyatamka hayo akitaka awe gumzo lakini jitihada hizo kama vile zimekunywa maji. Sasa namwona ameibuka kwenye video mpya ya Juma Jux. Yeye ndiye video vixen kwenye kazi ile. Sijui kama ni kazi ya zamani ama ya juzi. Ila inanikalia ya juzi sana. Lakini pia najua amekuwa akimmezea mate sana Jux. Na wajua tena Jux anavyopenda wa kubebeka (portable).

Mwangalie Huddah kisha mwangalie Ex wake Vanessa Mdee. Sijui kama umeipata picha.

Nimeshangaa kumwona Huddah akiwa video vixen kazi aliyowahi kusema hatafanya tena. Kazi iliyompa umaarufu. Kama unashangaa, basi nenda YouTube. Nina uhakika utakutana na video moja ya zamani yake akiwa na bonge la pengo mdomoni, sijui aling’oa jino hilo akifanyaje.

Ila ndio alikuwa Huddah origino, Huddah kienyeji. Lakini yote tisa, kumi ni dhahiri ana hofu ‘taaluma’ yake ipo kwenye kipindi cha lala salama.

Yupo radhi kufanya lolote arudi kwenye chati kama zamani. Kwa bahati mbaya yeye sio Kim Kardashian. Yeye ni demu wa kawaida sana.

  • Tags

You can share this post!

Alama za wagombeaji huru wa urais zazua hali ya kukanganya

KIKOLEZO: Edi Gathegi yule msee!

T L