DOMO: Eti Zari Hassan kavimba kichwa!

DOMO: Eti Zari Hassan kavimba kichwa!

NA MWANAMIPASHO

ACHA nianze kwa kusema hivi, inaumiza na kunisikitisha kuona soshiolaiti anatoka Afrika Kusini na kuja Kenya kukusanya hela kwa ajili ya promosheni.

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa taarifa, zitakuwa zimekufikia habari kuwa Zari Hassan alikusanya zaidi ya Sh2.5 milioni kwa ziara yake ya siku tatu mjini Kanairo wikendi iliyopita.

Taarifa yenyewe niliiandaa mimi baada ya kumfuatilia bibiye kwa siku mbili tukiomba mahojiano naye lakini aliamua kunionyesha u-diva. Licha ya kufahamu kabisa kuwa wanahahabari walikuwepo wakihitaji muda naye, aliamua kutukausha. Haina neno bado niliondoka na stori kwa kuwa nilikuwepo kwenye eneo la tukio alilolishinda kwa kutwa mbili.

Lakini wala hiyo sio ishu ninayotaka kuitoa moyoni. Kusema kweli nilitegemea mama wa miaka 41 tena aliyezalishwa mara tano, angelikuwa mwingi wa busara. Ila nilichokutana nacho kiliniacha kumshangaa. Kwa siku mbili mimi na mwenzangu kutoka Star tulikesha kwenye jumba moja la kifahari katika mtaa wa Runda Mumwe tukisubiri amalize shuti ili tupate fursa ya kumhoji. Taarifa za uwepo wetu alikuwa nazo. Ila hata baada ya kutukalisha kutwa nzima kwenye siku ya kwanza, alirudia tena hivyo siku iliyofuatia ambayo meneja wake alituomba tuje na kutuhakikishia Zari angetupa muda wake.

Aisee! Kama sio kwa heshima ya bosi wangu, wala sikuwa kabisa na dhamira ya kukimbizana na stori hiyo. Lakini mwisho wa siku nilipata kumwelewa japo kwa umbali ni mtu wa aina gani. Zari kavimba kichwa kisa, ustaa na inasikitisha kwa umri kama wake, anashindwa kuwa na busara za kumheshimu kila mtu. Mwanzo kabisa ana roho mbaya. Hata salamu za Mungu alishindwa kutupa na mara zote mbili alizotuona tukimnyemelea, alijifanya hatuoni. Nashukuru Ben 10 wake yupo tofauti. Kila alipotuona kwa siku hizo mbili, alihakikisha anatusabahi.

Na kama haitoshi siku ya pili aliyopaswa kutupa wasaa wa kumhoji, aliwahi kumaliza shuti mapema na alipofuatwa na meneja ili kututengea dakika kumi, bibiye aligeuka na kuwa mjeuri kwa kusema hawapendi wanahabari Wakenya kwa sababu wanapenda kupindisha mambo? Hivi ni kwa nini hakuitoa kauli hiyo siku ya kwanza? Tusingejisumbua kurudi. Na hata kama madai yake ni kweli, hivi kati ya wanahabari Wakenya na yule bloga maarufu wa kiBongo, Mange Kimambi ambaye wao hukesha wakilipuana vijembe, nani mbaya zaidi? Zari hakutaka kutupa mahojiano na ingelikuwa sawa kutuambia mapema ili tumwache na muda wake badala ya kutuhangaisha siku mbili mfululizo utadhani anatuadhibu kwa kumwibia kuku.

Hapa nilIpo nawaza, kama ndivyo alivyo na roho mbaya kwa wanahabari wasiomfanyia lolote, unafikiri atamfanyaje huyo Ben 10 wake? Sio bure amekuwa akiwabadilisha vibenten siku za hivi karibuni. Ukweli ni kuwa anawatumia kwa manufaa yake. Bibiye anajua anachuchujuka, umri unakwenda mbio na hivyo anahitaji kuwa na damu changa ili kuendelea kuwazengua mitandaoni. Nilipata fursa ya kumwona kwa ukaribu na wala zile picha za Insta zisikudanganye, kama ni makunyanzi, anayo sema picha hupigwa ukarabati na kumfananisha na binti wa miaka 20.

Zile picha za mapaja yake na mguu yanayomwonyesha akiwa amelainika, walai hayupo hivyo shangazi. Kwa ukaribu utaona kabisa ile michirizo ya ngozi inayosababishwa na mwili kuwa na mafuta mengi. Namhurumia dogo Ben 10 sababu atatafunwa kisha atemwe kama maganda ya miwa. Huko kujipendekeza nilioona akimbebea vibegi hadi vile vibeti vidogo, wala havitamwepushia shoka la bibiye atakapomchoka. Sasa nimeelewa kwa nini video yake ya ngono ilivujishwa. Zari ana roho mbaya na kama sivyo, basi ana roho chafu. Kujeni munipige!

  • Tags

You can share this post!

Kumbe wana doa!

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa meatloaf

T L