DOMO: Hilo zigo lina nini jamani?

DOMO: Hilo zigo lina nini jamani?

NA MWANAMIPASHO

HIVI lile zigo la Amber Ray lina nini haswa?

Nipo hapa kijiweni napitia picha za sista Insta nikiwaza.

Kwenye ukurasa wake walai utapenda yatakayokutana na macho yako. Picha na video za kichokozi, mashallah!

Sista kabarikiwa sijui kama origino au Mchina ila ukionacho kinaridhisha na kushibisha macho kabisa.

Hata wenzake wa jinsia yake watakuambia. Sista ana kishundu wewe, balaa!

Ana kiuno chembamba kama cha nyigu. Kisha upande wa juu taratibu ukutane na vile vilima. Sitaki kuamini vimesimama tisti kama vilima vya Taita. Lakini pamoja na yote bado, msupa anajua kuzipanga zikakupa mvuto.

Ongezea sasa na sura yake nzuri ya Kikamba. Tabasamu lake ambalo huna uhakika kama ni la kihuni au la dhati.

Halafu kichwani kakutundikia zile wigi zilizoundwa kwa mkia wa farasi. Ila subiri, huyu kwa jinsi anavyojua kuwatoanisha madume, wigi yake itakuwa ni origino. Yaani nywele za Wahindi au raia wa Thailand wanaofuga nywele zao kuwa ndefu na kuziuza kwa nchi zingine ili watu kama Amber waweze kuwakunywa kisawasawa.

Bibiye pia anajua kutupia pamba. Akiamua kupiga rinda, basi atahakikisha linabana kisawasawa ili kukupa picha kamili ya kazi ya Mungu. Ila Allah mbunifu wewe. Amini kabisa ukikutana na Amber akiwa kwenye mwonekano wake kama unaelekea ibada, basi kuwa na uhakika wa kutenda dhambi kwenye fikra zako.

Huyo mtoto wa watu kaiva, mwonekano wake hasa hayo makalio yamempa followers wengi wanaomfuata kufurahisha macho. Huku ndiko nzi wengi wamekufia kidondani, mmoja akiwa Jamal Roho Safi.

Wanasema ukiona vyaelea jua vimeundwa. Lakini tena waswahili wanatuambia, usihadaike na rangi ya chai, utamu wa chai ni sukari. Semi zote hizi kinzani zinaendana na hulka ya huyu mrembo.

Nakumbuka mapenzi yaliposhamiri kati ya Jamal na Amber, hatukujua kuwa jamaa alikuwa mume wa mtu.

Mapenzi yalinoga, Roho Safi akalishiwa mnofu hadi akawa na roho chafu, akamsahau mke wake Amira.

Mke wake ana mwonekano wake, ila kajiachilia kidogo. Wakenya wachokozi mtandaoni niliwaona wakimchamba kuwa ‘anakaa vile anataka’ na ndio sababu za jamaa kuibuka kwake Amber.

Juzi Jamal aliamua kumwomba msamaha hadharani. Akaandika hotuba ndefu niliyoisoma kidogo nisinzie. Ilikuwa ni hotuba ya dume linalojutia.

Dume lililogundua kuwa kile ni kishundu tu, wala hakina faida kubwa zaidi ya kumsitiri mumiliki wake anapoketi au kwenda msalani. Kimawazo sista hayupo kabisa. Hawezi kumwongeza mwanamume na kumfanya bora zaidi.

Atakupa kishundu ucheze nacho, upagawe, umwage hela zako na kisha kikiumana ataondoka na mzigo wake akiacha na hasara.

Kinachonisikitisha ni kuwa nzi wengi wanazidi kufia pale.

Jamal hakuwa wa kwanza, alikuwepo yule tajiri Zaheer Jhanda ambaye pia aliingia kwenye ndoa na sista licha ya kuwa na mke. Bahati dini yao inawaruhusu.

Jamal alishindwa kusoma kutoka kwa makosa ya mwenzake kuwa huyu binti ndoa sio kitu cha kumtishia, ataingia akukamue akuache.

Alipokuwa kwenye ndoa na Zaheer alibadili hadi jina na kuwa Mwislamu sijui aliitwa Maimuna au nani vile.

Nisichokielewa ni hichi,hawa nzi kila wanapofia kidondani, wote huwa wanalalamika sana. Zaheer alilalama, Jamal akalalama, yule mhuni wa Sierra Leone vile vile.

Sasa kuna huyu wa sasa sijui ni wakili.

Hivi ndugu zangu, hilo zigo la Amber Ray lina nini jamani? Mimi mbona naona limehudumiwa sana, bora tuliache tu. Au ndio wasemavyo Waswahili, kama tamu lamba?

You can share this post!

Wanne wapatikana na hatia ya kuua wakili Willie Kimani,...

Maafisa watatu wa polisi wapatikana na hatia ya kumuua...

T L