DOMO: Inasikitisha Omosh kashuka levo hizi!

DOMO: Inasikitisha Omosh kashuka levo hizi!

NA MWANAMIPASHO

KUNA bwana mmoja juzi kanikumbusha kuendelea kupambana na maisha, sababu siku hizi nguo hazianikwi kwenye jua na kama basi sitaki kuendelea kuanika nguo zangu kwenye jua kila nikifua, basi nitafute hela.

Kauli hii ndio tena imenishika mguu baada ya kuicheki ile video ya Omosh Kizangila akiombewa na pasta muhuni, Victor Kanyari. Sasa kama uliiona ile video ya Size 8 akijidai kukemea mapepo kutoka kwa watu kadhaa kanisani na ukaamini, basi hii ya Kanyari na Omosh utasadiki.

Sijui ni kwa nini wanapenda kufanya hivi vituko kwenye makamera. Hata Size 8 ambaye hivi majuzi tu alikuwa akitunengulia viuno na makalio, leo hii anadiriki kukemea pepo tena kwa kuiamrisha inyamaze, nazo zikatii. Enhe! Kawa Yesu nini?

Hivi vituko lazima atakua ameiga kwa watu kama Kanyari ili kuja kuwafumba navyo watu macho. Bibiye kawa pasta na anataka kutudhihirishia kwamba kweli ana nguvu za Mungu. Aisee!

Watu wanabeba kumbeba Mungu ufala.

Kanyari ameshatajirika kweli kwa kuwahadaa waumini wake kwa vimbwanga kama hivyo. Si wakumbuka zile mbegu zake za 310?

Kumwona akiigiza na Omosh eti akimfukuzia mapepo kisha jamaa anadondoka utadhani gunia la simiti, ilibaki kunichekesha.Lakini kwa jicho la tatu nikagundua hapa watu wapo kazi kusaka hela. Omosh na uzumbukuku wake lazima atakuwa alilipwa na huyo pasta muhuni kufanya vituko hivyo.

Lengo ni kutuonyesha kuwa ana upako wa Mungu kuwaneemesha watu wanaoonekana kuwa ovyo machoni mwa jamii. Ndio sababu alimfuata Omosh lizee la wake wawili ila akili za kitoto. Ni sawa ndio mishemishe za mjini, kusaka maisha sio rahisi kwa hiyo kila mja anajitahidi kufanya jambo hata kama hilo la kumdhihaki Jah.

Kituko cha Kanyari kilinikumbusha kile sawia cha Pasta Ng’ang’a mbaye naye alijirekodi akikemea mapepo yamwondokee Rose Muhando.

Tetesi zilidai kuwa mwimbaji huyo aliyepoteza nuru yake alilipwa Sh5,000. Sijui Omosh alilipwa shilingi ngapi ila ninachojua, sio wengi wetu waliopokea upuzi wao.

Inasikitisha kumwona Omosh akiwa mtu aliyeshuka hadi levo hizi. Ndio picha ya wasanii wetu wengi. Hawajielewi na ndio maana kila siku wanajitokeza kama ombaomba. Huyu Omosh tayari tushamchangia lakini ni dhahiri bado anahangaika. Alijengewa nyumba sitashangaa kusikia kauza. Hizi hela alizopewa na Kanyari sitashangaa kusikia zote zimeisha akiwa anakata maji. Ni picha ya kusikitisha, Sheikh!

  • Tags

You can share this post!

Aston Villa wamsajili beki Diego Carlos kutoka Sevilla

WANDERI KAMAU: Maombi yamedhihirisha tena unafiki wetu kama...

T L