Makala

DOMO KAYA: Namumisi Moustapha, aisee mwambieni arudi

November 15th, 2019 2 min read

Na MWANAMIPASHO

WANASEMA muziki mgumu ndiyo maana wapo wasanii wamekuja wakipotea.

Ila sikutegemea kabisa mshikaji wangu Colonel Moustapha aka ‘Uncle Ukwaju’ naye angezama.

Kumbukumbu za Uncle Ukwaju zimenijia baada ya kuibuka na taarifa kuwa jomba siku hizi kageuka shoga. Kwa ninavyomjua anavyopenda mademu, hapo ndipo mawazo yangu yalianza kurudi nyuma hadi toka nilipokuja kumfahamu Moustapha.

Kwa mtu uliyeanza kuusikiza muziki wa Kenya miaka mingi imepita, Moustapha hatakuwa mgeni kwako. Alikuwa mwanachama wa kundi la Deux Vultures lililosumbua sana miaka hiyo akiwa na Nasty Thomas ambaye hata nilipomulizia Moustapha, alisema hana habari zake baada ya kundi lao kusambaratika.

Deux Vultures ilipokufa, Moustapha mkali wa vishasha aliendelea kufanya muziki wake kama msanii solo na alikuwa akifanya vizuri tu.

Sasa Uncle Ukwaju, Uncle Mus, Mr Loboko aka MR Hakuna Ngendembwe ni kama vile kafulia kimuziki. Walai tena kama sio hizi madai za ushoga nilikuwa mwenyewe nishasahau alikuwepo.

Mara ya mwisho Moustapha kuachia ngoma nafikiri ni 2017. Alianza kupotea kimuziki baada ya kupata dili la kuwa mmoja wa waigizaji kwenye kile kipindi cha masoshiolaiti Nairobi Diaries.

Toka kipindi hiki Moustapha ni kama vile hajawahi tena kukanyaga studio. Maisha yake yanaendelea ila sio kwa kutegemea kipato cha muziki tena.

Nafahamu ana biashara za viatu na manguo kwa sasa. Pia kumewahi kuwa na tetesi kwamba alikuwa na ki shuga mummy kilichokuwa kikimweka mjini kutokana na shuguli yake nzito pale chumbani. Haikosi ndio sababu Moustapha anakeshaga gym. Moustapha ninamumisi kwa sababu nyingi sana.

Ni mmoja wa wasanii waliokuwa wakiichangamsha Showbizz yetu. Uncle Ukwaju anapenda vishasha na ubishi na hii ilikuwa ikitia ladha sana Showbizz. Kama unakumbuka penzi lake na msanii Marya lilipoingia mchanga, walitrendi sana. Moustapha kisha akaja kuingia kwenye bifu na CMB Prezzo anayedaiwa kuwa siku hizi kawa mlambaji poda. Mpaka leo halijaisha. Aliwahi kumwibia demu Prezzo demu mwenyewe ni huyu Huddah.

Lakini Moustapha aliachana na Huddah baada ya wiki mbili tu sababu sista alikuwa anaitisha hela nyingi kuliko uwezo wake Moustapha.

Nakumbuka Moustapha akizua kioja kwa zile picha chafu walizopiga na Huddah huku mkono wake Uncle Ukwaju akiwa ameulekeza ndani ya kaptura ya jeans ya Huddah kwa mbele huku nia ikiwa wazi alikuwa anataka kumshika yule nyau.

Nakumbuka Nyota Ndogo akicharuka sana baada ya kuziona picha zile kiasi cha kuzua maandamano na wanawake wengine kumkashifu. Lakini Huddah na Moustapha hawa ni viumbe ajabu.

Kama kuna kitu kimoja ninachofahamu bayana kuwahusu ni kwamba hawajali. Moustapha wa siku hizi hana hivi vimbwaga. Hatumskii tena. Vilikuwa vinasadia kuchangamsha gemu lakini pia kumsukumia kazi zake.

Au atakuwa kazeeka na ndio maana kapotea. Siku hizi hamna visanga tena. Willy Paul tushamchoka na visanga vyake vya kitoto.