DOMO: Mhesh asalimu amri ya KOT!

DOMO: Mhesh asalimu amri ya KOT!

NA MWANAMIPASHO

NAFIKIRI nishawahi kusema hapa na narudia tena, vitu vitatu ninavyoviogopa mimi; ni Mungu, uji moto na sasa KOT.

Amini usiamini KOT waliamua kushuka naye Riggy G, kisa staili yake ya mavazi na kweli Mhesh amesalimu amri.

Awali alijitanusha na kujifanya mbishi kwa kusema hajali anavyochambwa ilimuradi mkewe na wanawe wanapendezwa na hizo suti zake kubwa ninazohisi zimeshonwa na fundi wake M7.

Riggy G kwa ujeuri alisisitiza kuwa atavaa atakavyo cha msingi kwake ni mkewe Pasta D na wanawe.

Mwonekano wake kwa kweli unatishia kumtoa yeyote matumaini. Suti zake huwa ni za ovyo na nashukuru Jumanne katambua hilo.

Halafu mwili wake, pia ametambua unahitaji kufanyiwa kazi. Sasa baada ya nyie KOT kumpasha kwa kuvaa ovyo, Riggy G kaamua kuja na stori tofauti.

Anasema hakuwa na wakati wa kwenda kununua nguo wakati ule wa kampeni sababu alikuwa akiwindwa na wapambe wa serikali iliyoondoka.

Kwa maneno yake anasema alihitaji kujihakikishia usalama wake kwanza hivyo hangeweza kupata muda wa kuzurura kwenda kununua mavazi mapya. Ila katucheza hapa. Ikiwa alikuwa anapata fursa ya kuzurura kupiga kampeni ina maana vipindi hivyo usalama wake haukuwa hatarini? Lakini pamoja na hayo, mie nashukuru maamuzi yake mapya. Mwanzo amesema tumpe miezi mitatu halafu atawaalika tena KOT kupiga msasa fasheni yake. Kwa kipindi hicho kasema anakwenda kuyatupa mavazi yake yote hayo yanayomfanya afanane na waigizaji vibonzo kisha anunue mapya. Kubwa azaidi, anasema ameingia gym lengo likiwa ni kuhakikisha anapunguza kilo 10 kutoka 94 za sasa hadi 84. Hizi ni nguvu za KOT ujue.

Pamoja na ujeuri wake, Riggy G kweli kasadiki kuuza sura ni jambo la muhimu. Hesabu zake ni kuwa baada ya kupoteza kilo hizo 10, kisha na mavazi mapya yanayomsitiri vizuri, basi atatosha hata kushindana na mamodo wa kiume. Hilo nimependa sana.

Nataka nimfahamishe tu, mazoezi sio suala la kulikenulia meno. Kama kweli anajiamini kuwa mchakarikaji, basi achakarike kufanya mazoezi.

Kwa sababu ana pesa kama mchanga wa bahari, ningemshauri awaajiri wataalamu wa mazoezi ili wamsaidie kuwa kwenye shepu. Amkanye bibiye kuendelea kumlisha chapati, mandazi sababu hizo zimemvurugia shepu. Pengine kama KOT wasingelimkalia kikao, Jumanne pale uwanjani Kasarani tungetiwa aibu sana. KOT kwa kweli nimewainamia. Umbea wenu umefana. Nyie hatari!

  • Tags

You can share this post!

Jinsi unavyoweza kupunguza uzito na kuboresha afya

KIKOLEZO: Nabii aliyekataliwa kwao!

T L