DOMO: Msikizeni shangazi, ana neno!

DOMO: Msikizeni shangazi, ana neno!

NA MWANAMIPASHO

HAHA! Eti ‘That Shawry for Viagra’, mnasema kafanyaje tena? Nilipomwona shangazi yenu akitrendi kule Twitter juzi kati, kidogo sikuelewa.

Ishu ilianzia pale alipoonekana kushangaa na taarifa kuwa matatu zinaruhusiwa kupitia kwenye Expressway. Kwa wakazi jiji la Nairobi, mtakuwa mnaelewa kabisa jinsi barabara hiyo ilivyo.

Caroline Mutoko alianza kutrendi baada ya matatu moja kusababisha ajali kwenye kizuizi kimoja cha kuingia kwenye Expressway.

Bibiye akatweet akionekana kushangazwa na matatu kuruhusiwa kutumia barabara hiyo ya Mchina ambayo tutalipia deni hadi wengi wetu wa kizazi cha sasa tufe.

Sasa tweet yake ikawasha moto. Bwana KOT mkaamua kumkaanga shangazi yenu licha ya kuwa mafuta ya kupikia yamepanda bei, Aisee! hamkuogopa. Kwa siku mbili mfululizo, shangazi alikuwa akitrendi. Yaani hata taarifa za usajili wa Manchester United bado hazikutoboa kumng’oa kileleni.

Mimi mliponipotezea ni hapo mlipoamua kumpachika jina la ‘That Shawry for Viagra’. Hamjui ni jinsi gani nilivyohangaika kubaini mlichokimaanisha. Niliogopa kuuliza msije niita mshamba. Lakini bwana kuuliza sio ujinga, basi jana nikamaua kuulizia afisini na pale nikapata picha. Watu wawili niliowauliza afisini walibaki kunishangaa…

“Kwani hujui? Si kuna ile stori eti yeye ndiye yule demu aliyekutwa na Mutula”…

Mutula Kilonzo alikuwa wakili maarufu aliyeaga dunia 2013.

Baadhi ya uvumi ni kwamba mzee alikuwa kwenye mahusiano na Mutoko. Narudia tena ni uvumi, ukweli anaujua yeye Mutoko, na Muumba wake pamoja na mwendazake. Kifo chake kiliibua stori kibao tu na Mutoko kujipata kwenye stori hizo mimi sielewi. Lakini Wakenya walivyo, kwao lisemwalo lipo kama halipo basi subirini lipo njiani laja. Basi mlishaamua yeye ndiye mhusika wa viagra.

Lakini kando na chambo zenu, hivi hamwoni kama shangazi yenu ana hoja kwenye anachokisema. Amesisitiza kuwa hangependa kuona matatu zikiruhusiwa kutumia Expressway kwa sababu madere wa matatu ni watovu wa nidhamu. Hilo nakubaliana naye kwa asilimia 200%. Wao kuruhusiwa kuendelea kutumia Expressway kutasababisha madhara makubwa sababu kule hamna jam. Kama kwenye jam ndio watukutu na wakorofi vile, itakuwaje kwenye barabara kama ile?

Lakini pia shangazi yenu anasema, kama pia ni lazima matatu zitumie Expressway, basi zilazimishwe kuweka Speed Governor. Kwenye hili pia namuunga mkono. Ni kama vile anawapenda, anayajali maisha yenu. Kasema sisi ni watu tusio na nidhamu, hilo nalo kweli. Sisi ni watu wakorofi sana. Ingelikuwa Watanzania ingekuwa afadhali kidogo.

Haya bwana pamoja na mimi kumuunga mkono shangazi yenu, sio kwamba namfagilia sana na sijui kwa nini. Ila napenda mtu anapokuwa mwingi wa hoja na mchache wa maneno. Sasa yeye kwa maneno, kama chiriku. Ila nitamlaumu vipi wakati kawa mtangazaji wa habari miaka yote hiyo?Jamani eeh! Msikizeni shangazi ana neno pale!

  • Tags

You can share this post!

DOMO: Msikizeni shangazi, ana neno!

TAHARIRI: Vituko vya Nick, serikali vyatamausha Starlets...

T L