DOMO: Mtu asiniambie kuhusu mapenzi

DOMO: Mtu asiniambie kuhusu mapenzi

NA MWANAMIPASHO

NDIO maana kila siku ya maisha yangu, huwa siyachukulii mapenzi kwa uzito.

Sipendi kitu cha kunichanganya. Na kama kuna kitu kinachoweza kukuzengua kiasi cha wewe kutojitambua ni penzi.

Wiki nzima hii imeshamiri mada ya mapenzi. Iwe kiki, iwe matendo iwe nini, visa vimehusu mapenzi.

Nikianza na Kevin Mboya aliyetrendi Twitter baada ya kutangaza anakwenda Kwale kutoka Nairobi kumsapuraizi mpenzi wake kwa maua.

Siku tatu baadaye akatokea kwenye YouTube na kusema alikwenda kule ila amerudi akiwa amevunjwa moyo na kuahidi kupeana uhondo kwenye chaneli yake mpya ya YouTube.

Ila Wakenya wajanja, hawakusita kumchana jamaa, kama kweli kule Kwale alipatana na habari za kuvunja moyo, ilikuwaje aliweza kurejea Nairobi na maua yakiwa bado freshi. Sema kutubeba ufala. Kwa tukio hilo la kisingizio cha penzi mwenzenu kawa maarufu.

Kisha yupo Nicah The Queen na kiki yake ya kipuzi akimshtumu msanii wa Ohangla Emma Jalamo kwa kujaribu kuvuruga mahusiano yake. Mwisho wa siku wanaachia ngoma. Sijui utengenezaji wa kiki choka mbaya kama ile, kama utasaidia kuisukuma ngoma hiyo maana mtu kama mimi sina muda wa kufuatilia ngoma inayosukumwa na upuzi. Muziki mzuri hujiuza.

Halafu lipo lile tukio la Chiki Kuruka akimfurusha yule binti aliyekuwa akimnengulia mume wake Bien kwenye steji wakati wa shoo yake wiki iliyopita uwanjani ABSA Grounds Nairobi.

Binti wa watu alipanda jukwani akaanza kumzungulishia Bien makalio yake.

Nina uhakika kaka alikuwa anafurahia ule mtagusano hadi pale Chiki alipoona na msela akaamua kusonga mbali. Chiki akawaita mabaunsa kutoa ulinzi zaidi.

Sasa Bien kamtetea mkewe akisema alikuwa anatekeleza wajibu wake kama meneja — ambao ni wa kuhakikisha anamtengenezea mandhari mazuri ya kikazi. Sijamwamini Bien. Ndio mambo ya mapenzi sasa. Mapenzi husingizia chochote. Mapenzi kwangu mimi ni utapeli tu.

Kama mifano hiyo haitoshi kudhibitisha kuwa kweli mapenzi ni utapeli, nifafanulie hili. Ni vipi DJ Bonez anakiri kuwa hajui ni lini atamwoa Kamene Goro licha yake kumchumbia mwaka uliopita? Kaka kaulizwa juzi anapanga lini ndoa, akajibu “Harusi Gani…”

Tena akaongeza na kusema ni Mungu tu ndiye ajuaye harusi itatokea lini.

Nipo hapa mimi najiuliza, kama hajui lini anapania kumwoa Kamene basi sababu zake za kumposa na kumvisha pete ya uchumba ya bei mbaya Sh8,500 ilikuwa ya kazi gani? Kweli mapenzi kizunguzungu.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Bien atetea ‘wivu’ wa mkewe

Mtoto Asome: Wanafunzi 50 kujiunga na shule baada ya...

T L