DOMO: Wakati mwingine tuache ujinga

DOMO: Wakati mwingine tuache ujinga

NA MWANAMIPASHO

WAKENYA bwana. Yaani licha ya uchumi wetu ulivyo mgumu bado tu elfu nne wewe mliamua hamtakosa Nyege Nyege Festival.

Kwa kweli kama kuna watu wanaoshikilia msemo wa ponda mali kufa kwaja, basi ni Wakenya. Wakenya mbele ya sherehe hata leo ikitokea tarumbeta imepigwa ya kwenda mbinguni, wengi wataikosa safari hiyo ilimuradi kuna sherehe. Enhee! Kulikuwaje huko maana naskia hata bafu hazikuwepo?

Lakini leo sipo huko, nataka niwatoe upumba nyie wote mliomchana Juliani na Lilian wake wiki yote hii mitandaoni.

Hivi huwa ni wivu, au mnapenda tu kushoboka na kuzungumza utumbo pasi na kuwaza?

Iliniumiza nilipoona wengi wenu mkisambaza picha za Juliani akiwa amevalia kienyeji mkimlinganisha na Slay King Alfred Mutua na mkawa mnashangaa ni kwa nini Lilian alimwacha Mutua akamwendea rastaman.

Hivi ni mara ngapi nimewaambia hapa kwamba, hampaswi kuhadaika na rangi ya chai, utamu wa chai ni sukari. Chai ya maziwa sio tamu bila sukari.

Pamoja na kuwa Juliani hapendi kupiga luku kwa viwango mnavyovitaka nyie mahasidi viwembe, huyu ni mmoja wa wasanii wenye utajiri mkubwa sana.

Juliani kwa wachache wetu tuliobahatika kutangamana naye ni mtu ambaye hapendi mashauo. Alizaliwa na kulelewa Dandora. Anaelewa haswa maana ya kulala njaa ni nini au kukosa nguo.

Malezi yake hayakuwa kama yenu mliolelewa na maziwa ya Celerac.

Na hata baada ya kubarikiwa kupata mkwanja, Juliani hajawahi kuiacha asili yake. Ameshasema akifikia kufa hataki kuwa na mali zozote zile kwa jina lake. Kwa maana hiyo kwenye wosia wake atatoa mali zake zote kwa mashirika ya kuwasaidia watu. Hivi kwa nyie mnayedhani ni msoto, mnafikiri mtu anaweza kutoa kauli hii bila ya kuwa na chochote?

Wakati maceleb wengine wameishi kuwa omba omba, haijawahi kutokea Juliani akawaomba hata ndururu zenu zaidi ya ile posti yake ya kebehi aliyoposti akiwasimanga mumtumie hela eti mwanawe kakosa diapers.

Pamoja na luku zake hizo za kishamba, mnapaswa kuelewa kuwa Juliani hasumbuliwi sana na vitu vya dunia. Ilimuradi anapumua ana vazi la kumsitiri na halali njaa yeye na mkewe, basi maisha yake yapo sawa.

Lakini kama hamjui tu, Juliani ni staa mkubwa mwenye heshima yake na wala hahitaji heshima zenu. Hivi mnafikiri ni kwa nini alikuwa na ukaribu mkubwa na marehemu Bob Collymore na wala sio nyie mahasidi.

Collymore hakuwa mtu wa levo zenu na nyie mnaojiona mnaishi vizuri kumliko Juliani, hata mngelikuwa na nambari zake za simu hamngempata.

Alimthamini Juliani kwa sababu ni jamaa linalojitambua. Ndio maana hata baada ya Lilian kuondoka, alitua taratibu kwa msela na akadata. Halafu kwa taarifa yenu, vichuna wote ambao Juliani katoka nao ni watu wenye heshima zao. Hii ina maana kuwa anathaminika zaidi kuliko huyo slay king wenu anayesumbuliwa na presha ya ujana licha ya uzee.

Mwangalie Brenda Wairimu, alikuwa na jamaa kwa miaka saba sijui. Kabla yake Juliani aliwahi kutoka na Sage. Mademu wa nguvu tu tena wenye majina makubwa. Wewe pumba una nini cha kumzidi Juliani zaidi ya luku? Wakati mwingine turuhusu busara itawale, tusipende kuonyesha ujinga wetu.

  • Tags

You can share this post!

Mashirika yataka adhabu kali kwa wauaji wa wazee

Afrika huagiza kiwango kikuu cha fatalaiza, matumizi yakiwa...

T L