DOMO: Yani Insta Babes hawaishi visanga

DOMO: Yani Insta Babes hawaishi visanga

NA MWANAMIPASHO

WIKI hii imekuwa nzito kweli na yeye matukio kibao.

Sio kwa baadhi yenu kuibuka na picha za uchi za binti anayefanana na Azziad na kudai kuwa ni yeye.

Kweli wanafanana ila hakuwa yeye Azziad. Mkamfanya binti atrendi bure tu.

Kisha kifo cha Waziri wa zamani wa Elimu Profesa Magoha, wengine wenu mkaunda akaunti Twitter kwa picha na majina yake na kuzitumia kuwajibu wote waliotuma rambi rambi zao.

Halafu kuna ishu hiyo ya mcheshi 2Mbili kutandikwa na mkewe, mara kachomwa visu mara kafungiwa nje. Mwenzenu pamoja na umbeya wake ni mpole hajui kufokana na mtu. Sasa wengine wenu mumemkashifu kwa kukubali kipigo kutoka kwa mwanamke. Wengine mumetania eti jamaa ametandikwa hadi kafanana mke wake.

Huwa mna muda mwingi wa kufuatilia vitu vya kipuzi jamani.

Ila iliyokuwa sho-stopa kwangu ni hii ya huyo influensa aitwaye Esther Muthoni almaarufu Nairofey. Juzi Nairofey kaamka na malalamishi kibao baada ya ndoa yake kuvunjika. Kwa machungu alimshtumu aliyekuwa mume wake Yeforian kwa kumfanyia hujuma. Insta Babe huyo alidai kwamba amekuwa akiishi maisha yake ya kifahari kwa kujigharimia ili kumkingia mumewe asionekane kuwa mume bwege, akawa anasingizia kuwa ni mume wake ndiye aliyekuwa akigharimia maisha yake yale.

Kubwa hata zaidi Nairofey alidai kuwa Yeforian alimzengua na kumpelekea kusaini mkataba wa ndoa ufahamikao kama Prenup. Mkataba huu kwa kawaida matakwa yake huwa ni kwamba pale ndoa inapovunjika hakuna kugawana mali. Kila mtu mume na mke anasalia na mali aliyochangia kutafuta. Ndio hujuma kubwa anayodai kufanyiwa na Yeforian jambo lililomsukuma jamaa kufunguka.

Kilichonichekesha mimi ni kusikiliza uwongo wa dada huyu peupe. Tumekuwepo kipindi mapenzi yake na Yeforian yanaanza. Alikuwa demu wa kawaida sana. Wakati anakutana na msela jamaa tayari alikuwa anaishi maisha ya kizungu. Alikuwa tayari ana kazi nzuri kule Urusi kama mtaalumu wa masuala ya kompyuta. Akamchukua dada wa watu na kwa pesa zake akamgeuza kuwa mtu. Data zote hizi binti wa watu alikuwa akituwekea YouTube.

Kutokana na mahusiano yao kuwa ya mbali, Yeforian akaona bora amwoe binti wa watu ili aweze kwenda kuishi naye.

Baadaye wakahamia Dubai na ndiko Nairofey alipiga sherehe kinoma. Ndoa yao iliingia ngori baada ya Nairofey kuanza kuhanya kwa mujibu wa Yeforian.

Jamaa anasema kuna kipindi alikuwa mgonjwa akafanyiwa operesheni, alimwomba mkewe aliyekuwa Kenya aende kumcheki ila mrembo akakwara. Baadaye jamaa anasema aliamua kuja Kenya bila ya kumtaarifu na ndio akamfumania.

Akaja kubaini alikuwa akimchepukia na demu mwingine na ndio chanzo cha ndoa yao kuvunjika.

Sasa hapo ndio Nairofey kaja kugutukia nguvu ya ile Prenup baada ya msela kuomba talaka mahakamani na sasa Insta Babe hana amani.

Ndio tatizo la hawa Insta Babes. Nimependa msela alivyomkomoa dada wa watu. Sasa basi dada wa watu kajikuta hana kitu.

Kwa bahati nzuri msela kaamua kumwachia vitu vya nyumba ila mali zake zote Insta Babe hapati chochote.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Zuchu ‘ajishtaki’

Saba wafariki kwenye ajali barabarani

T L