• Nairobi
  • Last Updated June 2nd, 2023 8:14 PM
Demu adondokwa mate ex wake akivisha pete kipusa aliyedharau

Demu adondokwa mate ex wake akivisha pete kipusa aliyedharau

NA JANET KAVUNGA

MALINDI MJINI

MWANADADA wa hapa alidondokwa mate akishuhudia mpenzi wake wa zamani akifunga harusi na demu ambaye awali alikuwa akimdharau mbele ya jamaa huyo.

Kipusa alipata habari kwamba ‘ex’ wake alikuwa akifanya harusi ya kukata na shoka na akaamua kuhudhuria japo hakujua Bi harusi alikuwa ni nani.

Bi harusi alipofika, mwanadada alibaini ni demu ambaye alikuwa akimdharau sana mapenzi yake na Bw harusi yalipokuwa moto.

Alimgeukia rafiki yake aliyeandamana naye kwenye harusi hiyo na kumfichulia jinsi alivyokuwa akimdharau demu huyo mbele ya jamaa aliyekuwa akimuoa.

“ Siamini macho yangu eti huyu demu ndiye Bi harusi wa huyu jamaa. Nilikuwa ninamdharau sana na sikufikiria wanaweza kuwa wapenzi na hata kuoana. Nilijitupa kwa kumtema jamaa,” demu alisema na kufuatilia harusi hadi mwisho.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge washtuka KPLC huuziwa stima na shirika la...

Mackenzie, washukiwa wengine 17 kuendelea kuzuiliwa kwa...

T L