• Nairobi
  • Last Updated May 29th, 2023 9:37 PM
Faini ya jogoo 3, mbuzi 2 kwa kula uroda na jirani

Faini ya jogoo 3, mbuzi 2 kwa kula uroda na jirani

NA TOBBIE WEKESA

MATUNGU, MUMIAS

MWANADADA aliyeolewa maeneo haya alipigwa faini ya jogoo watatu na mbuzi wawili, baada ya kupatikana akila uroda na jirani.

Inasemakana kipusa aliamrishwa na wazee wa ukoo wa mumewe kulipa faini hiyo baada ya kufumaniwa peupe amekunjwa sawasawa na jamaa asiye mumewe.

Duru zinasema kipusa alipatikana katika nyumba ya jirani, iliyoko takribani kilomita moja kutoka kwa boma lake, na wazee wakaitwa.

“Tumekuwa tukisikia mambo yako tu. Leo tumepata ushahidi. Nenda kwenu utuletee jogoo na mbuzi wawili,” kipusa alifokewa.

Habari zinasema kipusa alijaribu kuomba msamaha huku akitoa sababu iliyopelekea yeye kumpakulia jirani asali lakini hakusikilizwa.

  • Tags

You can share this post!

Uongezaji thamani mazao ya kilimo ndio siri ya kuimarisha...

Matatu yagonga lori na kuua abiria wanane

T L