NA JANET KAVUNGA
MTWAPA MJINI
ILIKUWA sinema ya bure kwa wenyeji wa hapa kahaba mmoja maarufu eneo hili aliposimulia jinsi mteja wake alivyobadilika ghafla na kuwa jini kabla ya kutoweka.
Demu huyo alidai kwamba, alipata mteja aliyeahidi kumpa donge kwa huduma za usiku kucha.
Walikodi chumba cha kulala katika hoteli moja mjini na hali ilikuwa shwari hadi demu alipotekwa na usingizi.
“Nilipogutuka usingizini, nilijipata peke yangu. Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani lakini mteja wangu hakuwepo,” demu alieleza baada ya “kuokolewa” na wahudumu wa gesti.
Alisema alipata ujira wa huduma alizompa “mteja” huyo kwenye meza ndogo iliyokuwa katika chumba walichokodi.
Wahudumu na walinzi wa gesti hiyo pia walipigwa na mshangao kwa kuwa hawakumuona mteja wa demu akiondoka.