• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Kidosho na shemeji waingia mitini baada ya kunaswa na mzee wakilishana mahanjam

Kidosho na shemeji waingia mitini baada ya kunaswa na mzee wakilishana mahanjam

CHANGAMWE, MOMBASA

Na JANET KAVUNGA

JOMBI mmoja hakuamini kugundua kwamba mkewe alikuwa akichepuka na kaka yake.

Jamaa alidhani ukuruba wa mkewe na kaka yake ulikuwa wa mtu na shemeji yake, hadi pale alipodokezewa na jirani kwamba wawili hao wanaendesha uhusiano wa kimapenzi kisiri.

Alifahamishwa kwamba kakake huchovya mzinga wa mkewe wakati ameeneda kazini.

Mwanamume akachukua hatua kuthibitisha madai hayo. Akaweka mtego uliowanasa wawili hao peupe kwani aliwafumania katika hali ya kutatanisha ndani ya nyumba ya kaka yake.

“Jamaa alikasirika nusura achome nyumba waangamie wote wawili lakini akajizuia,” alieleza mdokezi wetu.

Inasemekana mkewe hakurudi nyumbani kuanzia siku hiyo huku kaka ya jamaa pia akiingia mitini.

***

Mama mwenye hasira amtandika mwenzake kunyemelea mumewe

EMALI, MAKUENI

NA JOHN MUSYOKI

VITA vilizuka katika mji huu wa eneo la Mashariki akina dada wawili walipotwangana mmoja akilaumu mwenzake kwa kumezea mate mumewe.

Inasemekana wanawake wa mtaani walikuwa na tabia ya kuvizia kimapenzi waume wa watu bila kujali.

Siku ya kioja, mama huyo alimfumania mumewe akizungumza na mwanadada fulani. Alimrukia kidosho kwa hasira na kumwangushia kichapo huku jamaa akiuma kona na kuingia mitini.

“Leo itakuwa funzo kwa visura kama wewe wanaonyemelea waume wa watu,” mama alisema huku akimtwanga kipusa ikabidi watu kuingilia kati kuwatenganisha.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi ya kuandaa mlo bora bila kutumia mafuta

Tume ya haki yakatazwa kushiriki kesi Shakahola

T L