Na JANET KAVUNGA
MALINDI MJINI
MWALIMU wa shule moja viungani mwa mji huu amejitenga na mimba ambayo mpenzi wake anadai alipata walipopashana joto siku ya wapendanao.
Mwanadada huyo anayeishi mjini Nairobi alimtembelea jamaa siku ya wapendanao na wakawa na siku mbili za mapenzi moto moto kabla ya kurejea jijini siku ya tatu.
Juzi, demu alimtumia jamaa ujumbe kumfahamisha habari njema kwamba alipata mimba kufuatia nderemo zao za valentino.
Hata hivyo, jamaa hakuchangamkia habari hizo akishuku kwamba mwanadada alimtembelea akijua alikuwa tayari ametungwa mimba na mwanamume mwingine jijini.
Alimwambia demu wazi kuwa “mimi sio mjinga wa kubebeshwa mzigo wa mwanamume mwingine na kama ulidhani utaniingiza boksi kwa kunipa uroda kwa siku mbili unajidanganya.”