NA JANET KAVUNGA
UKUNDA, DIANI
BUDA mmoja alikita kambi katika ploti moja mtaani hapa akimtafuta pasta amuombee baada ya kulemewa na masharti ya mganga.
Taarifa zinasema buda alizoea kupata huduma za mganga huyo kwa muda mrefu hadi pale mambo yalipozidi unga baada ya kupatiwa masharti makali.
Inasemekana jamaa alitaka hirizi za kumkinga asirogwe na watu wasiomtakia mazuri.
Hata hivyo, mganga alipodai kutumia nyumba ya jamaa huyo kutekeleza shughuli za uganga na kumtaka asimkaribie mkewe, jamaa alianza kuingiwa na baridi.
“Alisema alishuku mganga alipomtaka achukue likizo ya kutoshiriki tendo la ndoa na mkewe,” alisema mdokezi.
Hapo ndipo jamaa aliamua kmtafuta pasta maarufu mtaani amuombee.
Kwa kuwa pasta alikuwa safarini jamaa aliamua kumsubiri hadi akawasili na kumuombea.