• Nairobi
  • Last Updated May 29th, 2023 9:37 PM
Ni mguu niponye pasta akifuata waumini kwa mama pima kijijini

Ni mguu niponye pasta akifuata waumini kwa mama pima kijijini

Kimuka ,KAJIADO

Na TOBBIE WEKESA

KIZAAZAA kilizuka eneo hili mapolo walipoacha glasi zao za vinywaji na kuchomoka mbio baada ya kuona gari la pasta wao likiingia kwa boma la mama pima.

“Hili gari linafanana na la pasta. Anatafuta nini huku?” polo mmoja aliwauliza wenzake.Penyenye zinasema makalameni walikuwa na mazoea ya kuingia vijijini na kunywa pombe kisiri.Inadaiwa pasta alipopata fununu kuhusu mienendo yao, aliamua kuwawekea mtego.

“Walahi huyu ni pasta. Mguu saidia,” polo mmoja alifoka huku akichomoka mbio.Wenzake walimfuata nyuma huku walevi wengine wakibaki vinywa wazi.“Hakuna haja ya kutoroka. Endeleeni na starehe zenu,” pasta aliwaeleza.Mama pima aliwafuata mapolo huku akiitisha malipo.

“Mama usijali. Hao ni waumini wa kanisa langu. Nitakulipa,” pasta alimueleza mama pima.

You can share this post!

Gor, Homeboyz kupigania rekodi za kutoshindwa

TAHARIRI: Gor, Tusker hazikufaa kubanduliwa kombe la CAF

T L