Donnarumma atawazwa Kipa Bora Duniani

Donnarumma atawazwa Kipa Bora Duniani

Na MASHIRIKA

MLINDA-LANGO wa Paris Saint-Germain (PSG), Gianluigi Donnarumma, aliyesaidia Italia kushinda taji la Euro 2020, alitawazwa mshindi wa taji la Yashin Trophy kwa kuibuka Kipa Bora wa Mwaka kwenye tuzo za Ballon d’Or 2021.

Chelsea walionyanyua taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) walitawazwa Klabu Bora ya Mwaka.

Kiungo wa Barcelona, Pedri, 19, alishinda taji la Kopa Trophy kwa kuibuka Mchezaji Bora asiyezidi umri wa miaka 21. Aliwabwaga Jude Bellingham, Mason Greenwood na Bukayo Saka waliambulia nafasi za pili, tano na sita.

Wachezaji 14 kati ya 30 waliounga orodha ya wawaniaji wa tuzo ya Ballon d’Or walikuwa ni masogora wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Chelsea walikuwa na wawakilishi watano wakiwemo Jorginho aliyeambulia nafasi ya tatu, N’Golo Kante (5), Romelu Lukaku (12), Mason Mount (19) na Cesar Azpilicueta (29).

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City, walikuwa pia na wawakilishi watano – Kevin de Bruyne (8), Raheem Sterling (15), Riyad Mahrez (20), Phil Foden (25) na Ruben Dias (26).

Manchester United waliwakilishwa na wanasoka wawili – Cristiano Ronaldo (6) na Bruno Fernandes (21) huku Liverpool na Tottenham Hotspur wakiwakilishwa na Mohamed Salah (7) na Harry Kane (23) mtawalia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mwaura arejea rasmi kama Seneta Maalum

Kipusa Alexia Putellas wa Barcelona atawazwa mshindi wa...

T L