Dortmund wamtimua kocha Marco Rose baada ya msimu mmoja

Dortmund wamtimua kocha Marco Rose baada ya msimu mmoja

Na MASHIRIKA

BORUSSIA Dortmund wamemfuta kazi kocha Marco Rose baada ya msimu mmoja.

Baada ya kuagana na Borussia Monchengladbach, Rose aliongoza Dortmund kukamilisha kampeni za Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) msimu huu katika nafasi ya pili huku pengo la alama nane likitamalaki kati yao na mabingwa Bayern Munich.

Dortmund pia walibanduliwa kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na Europa League na wakadenguliwa na limbukeni St Pauli kwenye kipute cha German Cup.

Kwa mujibu wa taarifa ya Dortmund, usimamizi “utajadili mchakato wa kuteua kikosi kipya cha benchi ya usimamizi katika siku zijazo.”

Rose alisimamia mechi 47 za Dortmund na akaongoza kikosi hicho kushinda mechi 27 na kupoteza 16.

Dortmund walibanduliwa mapema kwenye hatua ya makundi ya UEFA baada ya kuambulia nafasi ya tatu nyuma ya Ajax na Sporting Lisbon. Walishuka kwenye ligi ndogo ya Europa League ambapo walidenguliwa na Rangers.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wahandisi waonya wakazi wa Ruiru dhidi ya kukaribia jumba...

Wanaraga wa Kenya Simbas wang’atwa na Boland ligi ya...

T L