Habari Mseto

DPP aelezea nia ya kutaka kufutilia mbali kesi dhidi ya Ongoro

February 14th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Mbunge wa Ruaraka Elizabeth Ongoro amefika mahakamani Nairobi ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP ameeleza nia ya kufutilia mbali kesi dhidi yake na washukiwa wengine 21 wanaoshtakiwa kwa kufuja pesa za ustawishaji eneobunge hilo.

Mahakama imefahamishwa Masha – mumewe Elizabeth – aliwalaghai washtakiwa wawili Thomas Muruka Dola na Morris Orongo Sh310,000 kuwasaidia kulipa dhamana.

Kufikia sasa wangali jela.

Hakimu mkuu Lawrence Mugambi amewaamuru Muruka na Orongo wapige ripoti polisi achukuliwe hatua kali.