Dressel aweka rekodi mpya kwenye uogeleaji wa 100m butterfly

Dressel aweka rekodi mpya kwenye uogeleaji wa 100m butterfly

Na MASHIRIKA

MMAREKANI Caeleb Dressel aliweka rekodi mpya ya dunia kwa kushinda dhahabu ya Olimpiki kwenye uogeleaji wa 100m butterfly mnamo Julai 31, 2021.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alisajli muda wa sekunde 49.45 baada ya kuwapiku Kristof Milak wa Hungary kwa sekunde 0.23.

Katie Ledecky wa Amerika alishinda dhahabu ya 800m freestyle kwenye Olimpiki kwa mara ya tatu mfululizo huku Kaylee McKeown wa Australia akizoa kwenye 200m wanawake backstroke. Noe Ponti wa Uswisi aliridhika na nishani ya shaba.

Kwingineko, Uingereza walizoa dhahabu ya nne ya uogeleaji kwenye Olimpiki na kuweka rekodi mpya ya dunia kwenye 4x100m mixed medley relay.

Kathleen Dawson, Adam Peaty, James Guy na Anna Hopkin walishinda fani hiyo kwa dakika 3:37.58.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Bei ya chai sasa yapanda kanuni mpya zikianza kuzaa matunda

Raila anavyosuka ODM na Nyanza tayari kwa 2022