Habari Mseto

Duale akemea polisi walioua watu wawili Garissa

July 27th, 2020 1 min read

BRUHAN MAKONG na FAUSTINE NGILA

Mbunge wa Garisaa Aden Duale amekemea utumiaji wa nguvu kupita kiasi kwa polisi kufuatia kuuawa kwa watu wawili kwenye soko la mifugo mjini Garissa.

Tukio hilolilizua maandamano ya wakazi wa mji huo ambapo polisi walilazimika kurusha vitoa machozi hewani.

Bw Duale alikemea kitendo hicho cha mauaji ya Aden Abdi Madobe na Muhiyadin Adow Ahibin na polisi huku akiomba Wizara ya Usalama wa Ndani kukamata waliohusika.

Polisi nchini Kenya wamekuwa na mtindo wa kuwaua na kuwadhulumu raia wasio na hatia katika miaka ya hivi karibuni.