Dybala aokoa Juventus kinywani mwa Inter Milan katika gozi la Serie A

Dybala aokoa Juventus kinywani mwa Inter Milan katika gozi la Serie A

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI Paulo Dybala alitokea benchi katika kipindi cha pili na kufunga penalti iliyowazolea waajiri wake Juventus alama moja muhimu dhidi ya Inter Milan kwenye Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Inter ambao ni mabingwa watetezi wa kivumbi hicho, waliadhibiwa mwishoni mwa gozi hilo baada ya beki Denzel Dumfries kumkabili visivyo mwanasoka Alex Sandro ndani ya kijisanduku. Kocha wa Inter, Simone Inzaghi, alionyeshwa kadi nyekundu kwa kuchemkia marefa wa mechi hiyo kwa sababu ya maamuzi hayo.

Edin Dzeko alikuwa amewaweka Inter kifua mbele katika gozi hilo la d’Italia baada ya kukamilisha krosi ya Hakan Calhanoglu. Awali, Napoli waliambulia sare tasa dhidi ya nambari nne AS Roma na kuwaruka AC Milan kileleni mwa jedwali la Serie A.

Inter kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu japo pengo la alama saba linatamalaki kati yao na Milan. Juventus wanakamata nafasi ya sita huku wakihitaji alama moja pekee kuingia ndani ya mduara wa nne-bora na kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao.

You can share this post!

Barcelona na Boca Juniors kupimana ubabe kwenye kipute...

PSG na Marseille waumiza nyasi bure katika Ligi Kuu ya...

T L