Dzeko afunga mabao mawili na kusaidia Inter Milan kupepeta Bologna katika Serie A

Dzeko afunga mabao mawili na kusaidia Inter Milan kupepeta Bologna katika Serie A

Na MASHIRIKA

EDIN Dzeko alifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake Inter Milan kupepeta Bologna 6-1 katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Lautaro Martinez aliwaweka Inter kifua mbele mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kupitia krosi ya Denzel Dumfries kabla ya Milan Skriniar kufunga goli la pili baada ya kuandaliwa pasi na Federico Dimarco.

Nicolo Barella na Matias Vecino walifunga mabao mengine ya Inter kabla ya dakika 60 za mchezo.Dzeko alipachika wavuni mabao mawili ya haraka katika dakika za 62 na 68 kabla ya Arthur Theate kuwafutia Bologna machozi mwishoni mwa kipindi cha pili.

Mbali na kocha Antonio Conte aliyewashindia ubingwa wa Serie A muhula jana, Inter waliagana na wachezaji kadhaa wa haiba kubwa, akiwemo Romelu Lukaku, kutokana na hali ngumu ya kifedha.

Ingawa hivyo, mabingwa hao watetezi hawajapoteza mchuano wowote wa Serie A chini ya mkufunzi mpya Simone Inzaghi.Kufikia sasa, kikosi hicho kinajivunia mabao 16 kutokana na mechi nne za ufunguzi wa Serie A, hii ikiwa rekodi nzuri zaidi kwa Inter tangu 1960-61.

  • Tags

You can share this post!

Bayern Munich waponda Bochum na kufikisha mabao 20 kutokana...

Mombasa Olympic Ladies FC yasajili mastaa 10 kupania kurudi...