EACC yaandama Sh1.9 bilioni za Waititu

EACC yaandama Sh1.9 bilioni za Waititu

NA JURGEN NAMBEKA

TUME ya Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) imeanzisha mchakato wa kurejesha mali yenye thamani ya zaidi ya Sh1.9 bilioni aliyojizolea Gavana wa zamani wa Kiambu, Bw Ferdinand Waititu.

EACC imeeleza kwamba, ilipata ripoti kuwa Bw Waititu alikusanya mali yenye thamani Sh1,937,709,376 .

Kulingana na EACC, mali hiyo haiambatani na vitega uchumi vyake. Ripoti ilieleza kuwa mali aliyokusanya Bw Waititu, aliyebanduliwa uongozini kama gavana wa Kiambu kati ya 2015 na 2020, inatiliwa shaka.

Uchunguzi uliofanywa na EACC, Bw Waititu alitumia afisi yake vibaya akiwa Mbunge wa Kabete na hata baadaye, alipochaguliwa kuwa gavana wa Kiambu mnamo 2017.

“Waititu alijihusisha na biashara zilizogongana kimaslahi na maslahi ya umma. Alitumia nafasi hii kukusanya mali ambayo ilizidi vyanzo halisi vya kipato chake,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.

EACC ilieleza kuwa Bw Waititu alijihusisha na ubadhirifu wa fedha za umma, kupitia kandarasi zilizojaa udanganyifu.

Ripoti zinaeleza kuwa, aliweka maslahi yake katika zabuni zilizopewa kampuni za kutoa huduma katika kaunti ya Kiambu.

Inasemekana kuwa, baada ya kulipwa, wanakandarasi wale walimtumia Bw Waititu mgao.

  • Tags

You can share this post!

Rais Jammeh kushtakiwa kwa utawala mbovu

Tutanasa magari yote ya serikali, Chebukati aonya wagombea

T L