EACC yagonga mwamba katika uchunguzi kuhusu vyeti feki vya elimu

EACC yagonga mwamba katika uchunguzi kuhusu vyeti feki vya elimu

Na LEONARD ONYANGO

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amekataa ripoti ya uchunguzi ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusiana na vyeti feki.

Bw Haji aliitaka EACC kuziba mapengo yaliyo kwenye ripoti ya uchunguzi kuhusu mwalimu wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Tabata, Kaunti ya Kisii, ambaye anadaiwa kutumia cheti feki cha masomo kujipatia ajira katika Tume ya Kuajiri Walimu (TSC).

Uchunguzi uliofanywa na EACC ulionyesha kuwa mwalimu huyo alitumia vyeti vya masomo vya watu wawili kabla ya kuajiriwa na TSC na amefundisha katika shule mbalimbali.

Faili ya EACC iliwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka mnamo Machi mwaka huu ikipendekeza mwalimu huyo afunguliwe mashtaka ya ulaghai.

Lakini Bw Haji aliirejesha kwa DPP akisema kuwa ilikuwa na mapengo na kuitaka EACC kufanya uchunguzi zaidi, kulingana na taarifa iliyochapishwa jana katika Gazeti Rasmi la Serikali na mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukala.

Waziri wa Michezo wa Kaunti ya Meru ambaye alidaiwa kughushi cheti cha shahada ya digrii kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Waziri huyo anadai kuwa alitunukiwa cheti cha digrii ya Uchumi na Chuo Kikuu cha Nairobi alipohitimu 2010. Aliwasilisha cheti hicho mbele ya Bunge la Kaunti ya Meru alipokuwa akipigwa msasa kabla ya kuapishwa kushikilia wadhifa wa uwaziri.

Uchunguzi wa EACC ulibaini kuwa cheti hicho kilikuwa feki lakini Mkurugenzi wa Mashtaka aliitaka tume hiyo kufanya uchunguzi zaidi na kuziba mapengo.

You can share this post!

Peru wakung’uta Paraguay na kutinga nusu-fainali za...

Kiwanda cha mananasi kujengwa Gatundu Kaskazini